Urembo : Kamati ya Miss Tanzania Yazindua msimu mpya wa Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2016,Jijini Arusha - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


4 Apr 2016

Urembo : Kamati ya Miss Tanzania Yazindua msimu mpya wa Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania 2016,Jijini Arusha


Mrembo wa Taji la Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima akakitambulishwa ukumbi kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016.


Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania mkoa wa Arusha. Katikati ni Mkurugenzi wa Mwandago Investment, Chris Mwandago ambaye ni muandaji mashindano ya Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini, na kulia ni Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia anasifika kwa kufanya mambo mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali kupitia kipindi chake cha 'Mimi na Tanzania', Hoyce Temu.


Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu ambaye alikua mgeni rasmi akizungumza jambo.


Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu ambaye alikua mgeni rasmi akikata utepe kuzindua mashindano hayo jijini Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia anasifika kwa kufanya mambo mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali kupitia kipindi chake cha 'Mimi na Tanzania', Hoyce Temu (kulia), Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kulia) na Mrembo wa Taji la Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima.


Yamoto Band ikifanya mambo yake jukwaani ndani ya ukumbi wa Triple A jijini Arusha.


Wadau wa tasnia ya urembo wakifurahia jambo.

Baada ya kupewa baraka jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 yamezinduliwa tena jijini Arusha na Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu katika ukumbi wa klabu ya Triple A jijini humo na zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali yaliyojiri katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) akimiminiwa kinywaji cha K-Vant wakati wakiingia na wadau wa tasnia ya urembo kwenye ukumbi wa Triple A jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 uliofanyika mwishoni mwa juma.
Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia anasifika kwa kufanya mambo mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali kupitia kipindi chake cha 'Mimi na Tanzania', Hoyce Temu (katikati) akiwa na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima wakikaribishwa ukumbini na kupewa kinywaji cha K -Vant ambao walikua wadhamini wa shughuli hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha.
Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia anasifika kwa kufanya mambo mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali kupitia kipindi chake cha 'Mimi na Tanzania', Hoyce Temu (kushoto) na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima wakifurahia kinywaji cha K-Vant.

Post Top Ad