TEHAMA : Clouds Media Group ikiongozwa na MD Joe Kussaga yatembelea nyumbani kwa Balozi Manongi, New York - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 24 April 2016

TEHAMA : Clouds Media Group ikiongozwa na MD Joe Kussaga yatembelea nyumbani kwa Balozi Manongi, New York


Mwakilishi wa kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Tovako Manongi akimkaribisha Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga nyumbani kwake siku ya Jumamosi April 23, 2016.
Mkurugenzi huyo alitembelea nyumbani kwa Balozi jijini New York akiongozana na baadhi ya wafanyakzi wake ambao walikuja nchini Marekani kwa ajili ya tamasha la Radio lililofanyika jijini Las Vegas. Picha na Vijimambo New York.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi akiwatambulisha maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa kwa Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bwn, Joseph Kusaga (hayupo pichani) siku ya Jumamosi April 23, 2016.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Bwn. Joseph Kusaga akitambulisha timu yake kwa Mhe. Balozi Tuvako Manongi.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi, mwakilishi wa kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bwn. Joseph Kusaga.
Mkurugenzi wa Clouds Medea Group, Bwn. Joseph Kusaga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Tuvako Manongi na mkewe.
Timu nzima ya Clouds Media Group iliyohudhuria Tamasha la Radio nchini Marekani ikiwa katika picha ya pamoja na Balozi Tuvako Manongi na mkewe.
Kutoka kushoto ni Saleh Mohammed, Daudu Lembuya, Dj Venture, Mhe. Balozi Tuvako Manongi, Mkurugenzi Joseph Kusaga, Mama Manongi, Dj Peter Moe na Jackson Joseph.
Kushoto ni Brightus Titus, Getrude Clement na NY Ebra wakiwa katika picha ya pamoja.

Siku hiyo pia lilifanyika kusanyiko la maDJ mbalimbali wa zamani waishio nchini Marekani ambao walikutana kwa nyama choma na kubadilishana mawazo. MaDj hawa ni wachache miongoni mwa wengi wanaounda kundi la Tanzania Djs Worldwide ambalo limeanza miezi mitatu iliyopita, na mpaka sasa lina wanachama wapatao 70. Kusanyiko lao la kwanza lilifanyika Escape One March 24 (lirejee hapa)


No comments:

Post a Comment