Sababu za UKAWA kususia hotuba hiyo ni hizi...
1. Serikali kufanya kazi bila kuwa na mwongozo wa utendaji wake na kazi kwa wizara mbalimbali jambo linaloonekana kuwa Serikali inafanya kazi kwa kauli za Rais na Mawaziri bila kufuata mwongozo wowote wenye msingi na uhalali wa kisheria kama inavyoelekezwa na kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Utekelezaji Majukumu ya Mawaziri SHERIA YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA MAWAZIRI (Ministers – Discharge of Ministerial Functions - Act, 1980 kinachosomeka “the President shall from time to time by notice published in the Gazette, specify the departments, business and other matters and responsibility for which he has retained for himself or he has assigned under his direction to any minister and may in that notice specify the effective date of the assumption of that responsibility…….”
2. Serikali kutoheshimu na kuzingatia Sheria zilizotungwa na Bunge kwa masuala ya fedha za umma kwa kuzingatia Ibara ya 63(3)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kifungu cha 41(1) cha Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015, Sheria ya Fedha za Umma wa mwaka 2001( Public Finacne Act, 2001) kifungu cha 18 (3) na (4) kinachoitaka Serikali kupeleka Bungeni bajeti ya nyongeza ( mini-budget) kwa ajili ya kupata idhini ya Bunge ikiwa fedha zilizoidhinishwa awali hazikutosha.
Wakatolea mfano wa bajeti ya maendeleo iliyokuwa imeidhinishwa na Bunge kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2015/16 ilikuwa ni shilingi bilioni 883.8 ambapo kati ya fedha hizo, fedha za ndani zilikuwa ni shilingi bilioni 191.6 lakini hadi kufikia mwezi Machi 2016 Wizara ilikuwa imeshapokea kutoka hazina shilingi bilioni 607.4 ikiwa ni fedha za ndani.
3. Serikali kulipoka Uhuru na Madaraka ya Bunge tofauti na Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayolitaja Bunge kuwa ndicho chombo kikuu katika Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake.
4. Serikali na uongozi wa Bunge kuwapoka wananchi haki yao ya kupata habari za Bunge kwa kuzuia mijadala Bungeni kurushwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa na vyombo vingine vya habari vya kujitegemea, ikiwa ni uvunjwaji wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Credit: Millard Ayo (for Video Clip)
No comments:
Post a Comment