Matukio : Waziri Lwenge Azindua mradi wa chanzo cha chemichemi ya kisimeni ,Mkoani Kilimanjaro - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


3 Mar 2016

Matukio : Waziri Lwenge Azindua mradi wa chanzo cha chemichemi ya kisimeni ,Mkoani Kilimanjaro

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru ,akimuongoza Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge alipofika kwa ajili ya uzidunzi wa mradi wa chanzo cha maji cha Kisimeni.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru ,akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge juu ya mradi wa chanzo cha maji cha Kisimeni .kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga.wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa MUWSA,Prof,Faustine Bee,(kushoto) na anayemfuatia ni Mkurugezi wa Halamshauri ya Manspaa ya Moshi,Jesh Lupembe.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru ,akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge juu ya mradi wa chanzo cha maji cha Kisimeni 
 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru ,akitoa maelezo ya hatua mbalimbali yanapo chukuliwa maji kutoka katika Chemichemi ya Kisimeni kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge alipofika kwa ajili ya uzidunzi wa mradi wa chanzo cha maji cha Kisimeni .
Meneja ufundi wa  Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi MUWSA,Mhandisi Paatrick Kibasa akimueleza Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Geryson Lwenge namna ambavyo maji yanayopatikana katika chemichemi ya Kisimeni yanavyotibiwa kabla ya kwenda kwa mtumiaji wa mwisho.
Waziri Lwenge akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael walipokutana katika uzinduzi wa mradi huo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Lwenge akitia saini katika kitabu cha wageni alipofika katika mradi wa Chemichemi ya Kisimeni kwa ajili ya uzinduzi.anayeshuhudia ni mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,Joyce Msiru.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Lwenge akiondosha kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa Maji wa chanzo cha maji cha Chemichemi ya Kisimeni.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Lwenge akiwasili katika viwamja vya shule ya sekondari ya Longuo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo watakaofaidika na uzinduzi wa mradi huo wa maji.
Vijana wa Skauti wakimvisha Skafu Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Lwenge alipowasili uwanjani hapo.
Vijana wa Skauti wakionesha umahiri wao mbele ya Waziri Lwenge.
Diwani wa kata ya Uru Kaskazini,Wilhad Kitally akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa chanzo cha maji chemi chemi ya Kisimeni.
Mameneja wa idara mbalimbali katika Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA,wakiwa katika uzinduzi huo.
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA,Prof Faustine Bee akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA,Joyce Msiru akitoa taarifa ya mamlaka hiyo kwa Mh,Waziri wa maji na umwagiliaji ,Mhandisi Geryson Lwenge pamoja na taarifa ya mradi wa maji ya Chemichemi ya Kisimeni ambao umetekelezwa ndani ya siku 100.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA,Joyce Msiru akikabidhi taarifa ya mamlaka hiyo kwa Mh,Waziri wa maji na umwagiliaji ,Mhandisi Geryson Lwenge.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini ,Anthony Komu akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Geryson Lwenge akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji yanayotokana na Chemichemi ya Kisimeni.
Wanafunzi wa Shule ya msingi ya Longuo wakitoa burudani ya wimbo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji wa Kisimeni.
Walimu wa shule ya msingi Longuo wakiimba shairi wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Mkurugenzi wa MUWSA ,Joyce Msiru akiwatunza waimbaji wa kikundi cha Msanja duzi kilichotoa burudani katika uzinduzi huo.
Mkaguzi wa Mahesabu wa ndani wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA,Benson Maro akiwatunza waimbaji wa kikundi cha Msanja.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Lwenge akizindua rasmi mradi wa maji katika kata Uru kaskazini.
Waziri Lwenge akimbebesha ndoo mmoja wa wakazi wa Longuo mara baada ya kufanya uzinduzi wa mradi huo.
Mgeni rasi katika uzinduzi huo ,Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Geryson Lwenge akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi,mameneja wa mamlaka hiyo na viongozi wengine waliofika katika uzinduzi huo.
Wakuu wa wilaya ,Anhtony Mtaka,(wilaya ya Hai) Novatus Makunga (wilaya ya Moshi mjini ) na Mbunge wa Moshi vijijini Anthony Komu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo.

Na Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini.

Post Top Ad