Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Hamis Kigwangalla(katikati) akielekezwa
jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom
Tanzania,Rosalynn Mworia(kulia)wakati alipowasili katika hafla ya
uzinduzi wa Mradi wa Moyo awamu ya Pili unaofadhiliwa na Vodacom
Foundation iliyofanyika wilayani Sengerema mkoani Mwanza juzi,kushoto
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo,Ian Ferrao.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Vodacom nchini, Balozi Mwanaidi Maajar akihutubia katika
uzinduzi wa Mradi wa Moyo awamu ya Pili unaofadhiliwa na mtandao wa simu
nchini Vodacom katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika wilayani Sengerema
mkoani Mwanza juzi.
Mkurugenzi
wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akihutubia katika uzinduzi wa Mradi wa
Moyo awamu ya Pili unaofadhiliwa na mtandao wa simu nchini Vodacom
katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika wilayani Sengerema mkoani Mwanza
juzi.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Hamis
Kigwangalla akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Moyo
awamu ya Pili unaofadhiliwa na Vodacom Foundation iliyofanyika wilayani
Sengerema mkoani Mwanza juzi.
Mkurugenzi
wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Hamis Kigwangalla katika
uzinduzi wa Moyo awamu ya Pili unaofadhiliwa na Vodacom Foundation
uliofanyika juzi katika Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza juzi.
Mkazi
wa Sengerema mkoani Mwanza, Lawrencia John akimuonyesha Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Hamis
Kigwangalla,Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Foundation, Balozi Mwanaid
Sinare Maajar, Mkurugenzi wa Vodacom nchini, Ian Ferrao(kulia) mtoto
wake Mwalu John aliyejifungua baada ya kupata msaada wa mradi wa Moyo
unaofadhiliwa na Vodacom Foundation jana katika uzinduzi wa Mradi huo
awamu ya pili mkoani humo.
Kaimu
Mkurugenzi wa USAID nchini, Bethany Haberer akisoma hotuba wakati wa
hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Moyo awamu ya Pili unaofadhiliwa na
Vodacom Foundation iliyofanyika wilayani Sengerema mkoani Mwanza juzi.
NAIBU
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dk. Hamis Kigwangala amezindua mradi wa kutokomeza vifo vya akina mama
wajawazito na watoto wachanga nchini,Mradi huo umezinduliwa jana
wilayani Sengerema mkoani Mwanza ambapo unafadhiliwa na taasisi ya
Vodacom Foundation kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa ya
USAID,Path Finder na Touch Foundation.
Mradi
huu ambao unajulikana kama”MOYO”awamu ya pili umelenga kuunga mkono
jitihada za serikali za kuboresha sekta ya afya nchini na adhma ya
kutokomeza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga nchini.
Akiongea
wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika mjini Sengerema Naibu Waziri
wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis
Kigwangala amesema kuwa mradi huu unaenda sambamba na malengo ya
serikali ambayo imejipanga kuhakikisha matukio ya vifo vya akina mama
wajawazito na watoto wachanga vinavyojitokeza wakati wa kujifungua
kutokana na ukosefu wa huduma za matibabu vinatokomezwa.
“Katika
kukabiliana na tatizo hili ambalo limetukutanisha hapa siku ya leo na
kuboresha huduma za matibabu nchini,serikali inatarajia kujenga wodi za
akina mama wajawazito katika vituo vyote vya Afya nchini vilivyopo
vijijini na mijini hivyo nawapongeza kwa kuiunga mkono serikali na natoa
wito kwa wananchi wote kuelewa jitihada hizi na kuvitumia vituo hivi na
huduma hizi ili kufanikisha lengo lililokusudiwa”.Alisema Dk. Hamis
Kigwangala.
Mkurugenzi
mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao amesema tangu mradi wa MOYO
awamu ya kwanza ulianza kutekelezwa mwaka 2009 na umefanikiwa
kuandikisha wanawake zaidi ya elfu 16,000 katika vituo vya afya, na
kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na Watoto zaidi ya 450.
Alisema
zipo baadhi ya changamoto kadhaa za baadhi ya akina mama wajawazito
kutojifungua katika vituo vya Afya, ambapo licha ya changamoto hizo
mradi huo umewezesha mafunzo kwa wahudumu wa Afya wa ngazi ya Jamii
wanaopita kila kaya kutoa elimu, ili kubadili mitazamo hasi ya baadhi ya
akina mama kutofika kwenye vituo vya afya kupatiwa huduma za uzazi.
“Kupitia
mradi huu ambao pia umelenga kurejesha fadhila kwa wateja wetu
tutagharamia usafiri wa akina mama wajawazito kupitia huduma ya M-Pesa
kama ambavyo ilikuwa kwenye awamu ya kwanza ya mradi ili waweze kufika
kwenye vituo vya afya kupata matibabu haraka pindi patakapohitajika
msaada “,Alisema.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Vodacom Foundation, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar, amesema
pamoja na mafanikio ya kiafya yaliyopatikana kwa kukabiliana na
ugonjwa wa Fistula na huduma ya ujumbe mfupi wa maneno ya kuelimisha
akina mama masuala ya uzazi kupitia mradi wa WAZAZI NIPENDENI kusaidia
akina mama wengi, vilevile zoezi hilo limekuwa likiviwezesha vikundi vya
kuweka na kukopa vya Wanawake na kuwapatia mafunzo ya kuwawezesha
kijikwamua kiuchumi.
“Kupitia
matumizi ya teknolojia ya huduma za simu za mkononi, kampuni imeweza
kuboresha maisha ya wananchi.Nawapongeza wadau wote ambao tumekuwa
tukishirikiana nao hasa Shirika la Msaada la watu wa Marekani (USAID).
Mkazi wa Sengerema Mwanza Lawrencia John,
ambaye ni mmoja wa wanawake walionufaika aliupongeza mradi huu na
kusema ulimsaidia alipokuwa kwenye hali ya uchungu wakati wa kujifungua
mtoto wake wa kwanza. Alipopiga simu aliweza kusaidiwa mara moja na
amejifungua salama kabisa na anatoa wito kwa wadau wengine waweze
kujitokeza kunufaika na huduma hii.
No comments:
Post a Comment