Matukio : Majambazi Wawili Wauawa na Jeshi la Polisi , Jijini Arusha. - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


15 Mar 2016

Matukio : Majambazi Wawili Wauawa na Jeshi la Polisi , Jijini Arusha.

Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog, Arusha.

Jeshi la polisi mkoani Arusha mnamo.tar 12/3/2016 limewaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambao walipanga kwenda kuvamia.kituo cha AVRDC kwa lengo la kuiba ambapi kituo hicho.kinajihusisha na utafiti wa kilimo nakipo eneo la.SADC kata ya Seela Sing'isi wilayani Arumeru.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas akizungumza na waandishi wa habari leo amesema kuwa jeshi lilipata taarifa kutoka kwa wasiri wao na wao waliweka mtego wa kuwakamata watu hao ilipofika majira ya saa tano na nusu usiku walijitokeza watu 4 waliovaa makoti marefu polisi waliwatilia shaka kuwa ndio waliotajwa katika tarifa ya msiri wao.

Kamanda amesema kuwa kati ya watu wale 4 wawili kati yao walitoa silaha walizokuwa wamezificha kwenye makoti.na.kuanza kuwashambulia askari,ndipo askari wakaanza kukabiliana nao kwa weledi na kufanikiwa kuwajeruhi wawili kati yao na wengine wawili walifanikiwa kukimbia nakutokomea gizani.

Polisi waliwapekua majeruhi na na waliwakuta na silaha mbili aina ya Shortgun,ya kwanza ina namba L814574, na CAR 69390 PUMP ACTION,ambayo baadae iligunduliwa kuwa iliporwa kituo cha Afya kinachomilikiwa na masista kinachojulikana kwa jina la Tumaini Health Center tarehe 25/02/2016  kilichopo kata ya Nkoaranga ,Na silaha ya pili ina namba TZ CAR 39046 pia iliokotwa kofia iliyokuwa na risasi 8za SHORTGUN. Bunduki zote mbili zimekamatwa vitako na Mitutu.

Kamanda Sabas amesema majeruhi walifariki wakiwa njiani wakipelekwa.hospitali ya Mountmeru kwa matibabu,miili ya marehemu hao imehifadhiwa hospitali ya Mountmeru kwaajili ya uchunguzi nautambuzi toka kwa ndugu na jamaa zao wa karibu.

Post Top Ad