Filamu : Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akabidhiwa Tunzo ya Msanii Bora Afrika - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


15 Mar 2016

Filamu : Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akabidhiwa Tunzo ya Msanii Bora Afrika

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wasanii wa Film wa hapa Nchini baada ya kukabidhiwa Tunzo ya mshindi Bora wa Film ya Kiswahili East Afrika (AMVCA) na Tunzo ya Kiswahili Afrika iliyofanyika Nchini Nigeria, hafla hiyo iliyofanyika March 14,2016 Oysterbay Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Tunzo ya mshindi Bora wa Film ya Kiswahili East Afrika (AMVCA) iliyofanyika Nchini Nigeria kutoka kwa mshindi wa Film hiyo Msanii Elizabeth Michael (Lulu) wakati wa hafla fupi iliyofanyika Oysterbay Dar es salaam March 14,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Tunzo ya mshindi Bora wa Film ya Kiswahili Afrika iliyofanyika Nchini Nigeria kutoka kwa mshindi wa Film hiyo Msanii Single Mtambalike (RICHIE) wakati wa hafla fupi iliyofanyika Oysterbay Dar es salaam March 14,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Filamu Nchini Single Mtambalike (RICHIE) na Elizabeth Michael (LULU) baada ya kupokea Tunzo za wasanii hao walizoshinda Nchini Nigeria, hafla hiyo iliyofanyika March 14,2016 Oysterbay Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katikati akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Filamu Nchini Single Mtambalike (RICHIE) na Elizabeth Michael (LULU) na Wasanii wengine baada ya kupokea Tunzo za wasanii hao walizoshinda Nchini Nigeria, hafla hiyo iliyofanyika March 14,2016 Oysterbay Dar es salaam.(Picha na OMR).

Post Top Ad