Bungeni : Spika afungua mkutano kati ya baadhi ya wabunge na wadau wa afya - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


7 Mar 2016

Bungeni : Spika afungua mkutano kati ya baadhi ya wabunge na wadau wa afya

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Afya kutoka Mfuko wa Dunia wa Afya Bw.Svend Robinson. Walikuwa wakizungumza kabla ya kuanza kwa mkutano uliowahusisha baadhi ya Wabunge na wadau wa Afya. Mkutano huo ulilenga kujadili kuhusu uwekezaji katika Sekta ya Afya na ulifanyika tarehe 3 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na baadhi ya Wabunge waliohudhuria mkutano wa pamoja na wadau wa Afya kujadaili kuhusu uwekezaji katika sekta ya Afya jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa pili kushoto), Naibu Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Hamis Kigwangala pamoja na Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Afya kutoka Mfuko wa Dunia wa Afya Bw.Svend Robinson wakifuatilia mazungumzo juu ya uwekezaji katika sekta ya Afya. Anayezungumza ni Mwakilishi wa Shirika la Afya hapa nchi Dkt Rufaro Chatora.
Baadhi ya Wabunge na Wadau wa Afya wakifuatilia mazungumzo juu ya uwekezaji katika sekta ya Afya hapa nchini.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akihutubia wadau mbalimbali wa Afya waliokutana kujadili juu ya uwekezaji katika Sekta ya Afya hapa nchini.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (kushoto) Mwakilishi wa Shirika la Afya hapa nchi Dkt Rufaro Chatora (katikakati) na na Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Afya kutoka Mfuko wa Dunia wa Afya Bw.Svend Robinson wakijadili jambo mara baada ya ufunguzi wa Mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Afya kujadili juu ya uwekezaji katika Sekta ya Afya hpa nchini. (Picha na Ofisi ya Bunge)

Post Top Ad