Teknolojia : Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania atembelea Clouds Fm na EFM Radio - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


20 Feb 2016

Teknolojia : Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania atembelea Clouds Fm na EFM Radio

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(kulia) pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakimsikiliza Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga(watatu kulia) alipokuwa akiwafafanulia jambo juu ya studio ya kurushia vipindi vinavyofanywa na kituo hicho, wakati wa ziara maalum iliyofanywa na Uongozi wa kampuni hiyo kwa ajili ya mafunzo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho kilichopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga (kushoto) na Mkurugenzi wa Vipindi wa kituo hicho, Ruge Mtahaba (kulia) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,( katikati ) alipokuwa akifafanua jambo juu ya utendaji mzuri wa kituo Clouds TV na Clouds FM, wakati alipouongoza Uongozi wa kampuni hiyo kutembelea makao makuu ya kituo hicho jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,(kulia ) akimsikiliza Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mtahaba(kushoto) alipokuwa akimuelezea jinsi shughuli mbalimbali za utangazaji zinavyoendeshwa na kituo hicho,wakati wa ziara maalumu iliyoongozwa na Mkurugenzi huyo kutembelea kituo hicho jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao( kushoto ) alipotembelea makao makuu ya kituo hicho jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho,katikati Materi Mushi.
Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Sebo(kushoto)akiwafafanulia jambo juu ya studio ya kisasa ya EFM, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia (katikati) Wakati wa ziara maalum ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam,kulia ni Mfanyakazi wa radio hiyo Kasampaida.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(kulia) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Redio ya EFM,Francis Ciza (Majey) baada ya Uongozi wa Vodacom Tanzania kutembelea ofisi hizo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(katikati) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia(kushoto)wakioneshwa na Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio ya EFM, Denis Sebo progaramu mbalimbali za vipindi vinavyozalishwa na redio hiyo,wakati wa ziara maalum iliyofanywa kituoni hapo na Uongozi wa Vodacom Tanzania kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam.

Post Top Ad