Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango (Katikati) akiwakabidhi
Naibu waziri wa katiba na sheria, Amon Mpanju(kulia) na Mtendaji mkuu
wa Mahakama Hussein Kattanga cheki ya shilingi Bilioni 12 na milioni mia
tatu ikiwa ni kutimiza ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Josef Magufuli
aliyoahidi siku alipokuwa mgeni rasmi siku ya Mahakama hapa nchini ikiwa
ni siku tano tuu tangu siku ya kuahidi.
Waziri wa Fedha Mipango, Philip Mpango (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kutimiza ahadi aliyoiahidi Rais Dkt. John Pombe Josef Magufuli alipoahidi katika maadhimisho ya siku ya mahakama hapa nchini. Kulia ni Naibu waziri wa katiba na sheria, Amon Mpanju na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.
Mtendaji mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga (kushoto)akimshukuru Rais Dkt. John Pombe Josef Magufuli kwa kutimiza ahadi yake aliyoiahidi siku ya maadhimisho ya siku ya mahakama. kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WIZARA
ya Fedha na Mipango imetoa sh.bilioni 12.3 kwa ajili shughuli za
mahakama ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli
aliyoiahidi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mahakama.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha na
Mipango, Dk. Philip Mpango amesema fedha hiyo imetolewa kwa kutimiza
ahadi ya Rais ya uendeshaji wa shughuli za mahakama.
Mpango
amesema kuwa ahadi ya Rais ilikuwa ni ya siku tano ambazo zimetimia kwa
kutoa hundi ya sh.bilioni 12.3 ambazo zitakwenda kufanya kazi
iliyokusudiwa.
Amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango kutokana na ahadi hiyo imefanya kuweka wazi juu ya fedha hizo kwa waandishi wa habari.
Nae
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju amesema
lengo ni kuongeza kasi kwa mashauri yaliyopo kuondoshwa pamoja na
waliokwepa kodi yashughulilikiwe.
Ahadi
ya Rais ilitolewa baada ya maombi ya Jaji Mkuu, Othman Chande katika
maadhimisho ya kuanza kwa mwaka wa mahakama kudai kuwa wana uhaba fedha
za maendeleo katika kuweza kuendesha shughuli za kimahakama.
Naibu
waziri wa katiba na sheria, Amon Mpanju akisaini dafari la wageni mara
baada ya kuwasili katika ofisi za wizara ya fedha na mipango jijini Dar
es Salaam.
Mtendaji
mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipowasili katia ofisi za wizara ya fedha na mipango jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment