Matukio : Mwili wa Mbunge Leticia Nyerere wawasili Dar, Mazishi Kufanyika Butiama,Mkoani Mara - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

Tuesday, 19 January 2016

demo-image

Matukio : Mwili wa Mbunge Leticia Nyerere wawasili Dar, Mazishi Kufanyika Butiama,Mkoani Mara


1
 Askari wa Bunge wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere aliyefariki nchini Marekani alikokuwa akitibiwa mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Mwili huo kesho utaagwa nyumbani kwa Mwalimu Nyerere Msasani  kabla ya kusafirishwa kwenda Butihama mkoani Mara kwa mazishi yatakayofanyika keshokutwa.
2
 Mwili huo ukiingizwa kwenye gari maalumu katika uwanja huo.
IMG_5307
 Ndugu jamaa na marafiki wakijadiliana jambo wakati wa kuupokea mwili huo.
IMG_5322
 Ndugu, jamaa, marafiki na watoto wa marehemu wakisubiri kuupokea mwili wa mpendwa wao.
IMG_5324
 Mume wa marehemu, Madaraka Nyerere akizungumza na wanahabari baada ya kuupokea mwili huo uwanjani hapo.
IMG_5325
Mtoto wa marehemu (kulia), akifarijiwa na mmoja wa ndugu wakati wakienda kupanda gari kabla ya kuondoka uwanjani hapo.

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *