Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula amesema kuwa Serikali
imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji, hivyo alitoa wito kwa
wafanyabiashara kutoka Qatar kutumia fursa lukuki za uwekezaji
zinazopatikana hapa nchini.
Balozi
Mulamula aliyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa katika hafla ya
kuadhimisha Siku ya Taifa ya Qatar iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt
Regence, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam jana.
“Tanzania
imeweka mazingira wezeshi ya uwekezaji katika sekta mbalimbali kama
vile kilimo, madini, uchukuzi, elimu, afya, nishati, wanyamapori, mafuta
na gesi, hivyo natoa wito kwa ndugu zetu wa Qatar watumie fursa ya
uhusiano mzuri tulionao kuja kuwekeza nchini”, Balozi Mulamula alisema.
Balozi
Mulamula aliendelea kusema kuwa Serikali inaelekea katika uchumi wa
gesi na ina matumani makubwa ya kufaidika na uzoefu wa mshirika wake
Qatar ambayo ni mmoja wa wazalishaji wakubwa wa gesi duniani.
Suala
lingine ambalo Katibu Mkuu aliligusia ni umuhimu wa Tanzania na Qatar
kuunganisha nguvu ili kutumia rasilimali fedha na ardhi zilizopo
kuimarisha sekta ya kilimo kwa madhumuni ya kuodoa changamoto za usalama
wa chakula kati ya nchi hizi mbili.
Kwa
upande wake, Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Abdulla Jassim Al Maadadi
pamoja na mambo mengine, aliongelea suala la Qatar kuwa mwenyeji wa
mashindano ya mpira wa miguu wa Kombe la Dunia kwa mwaka 2022. Alisema
miradi mingi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo inatarajiwa
kukamilika mwaka 2020. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara,
mtandao wa reli, viwanja vya mpira, viwanja vya ndege na nyumba za
makazi.
Alisema
miradi hiyo ni mikubwa hivyo inahitaji wafanyakazi wengi kutoka sehemu
mbalimbali duniani na aliahidi kuwa watu watakaokwenda kufanya kazi
nchini humo, haki zao zitalindwa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda
na Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akizungumza kwenye hafla ya
kuadhimisha ya Siku ya Taifa la Qatar kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi
Augustine Mahiga. Katika maadhimisho hayo, Balozi Mulamula alisitiza
umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar hususan
katika sekta za kiuchumi na biashara.
Sehemu ya Mabalozi na wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani)
Balozi Mulamula akiendelea kuzungumza
Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Abdallah Jassim Mohamed Al-Maadadi naye akizungumza katika maadhimisho hayo.
Sehemu nyingine ya Mabalozi waliohdhuria hafla hiyo.
Sehemu
ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bw. Hangi Mgaka (wa kwanza kulia), na
Bw. Batholomeo Jungu (wa pili kutoka kulia) nao wakimsikiliza Balozi
Al-Maadadi (hayupo), katika maadhimisho hayo.
Balozi
Mulamula (wa pili kutoka kulia), Balozi wa Qatar nchini (wa tatu kutoka
kulia), Balozi wa Demokrasia ya Kongo, Mhe. Juma Mpango (wa nne kutoka
kushoto), Balozi wa Oman nchini, Mhe. Soud Ali Bin Mohamed Al Rugaishi
(wa kwanza kushoto), Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), Mhe.
Abdulla Ibrahim Ghanim Al suwaidi (wa pili kutoka kushoto) wakishiriki
tendo la kukata Keki ya maadhimisho ya Siku ya Taifa la Qatar.
Balozi Mulamula akizungumza na Balozi Al - Maadadi.
Balozi
Mulamula akimtangaza mshindi wa bahati nasibu iliyochezeshwa hapo jana,
mshindi huyo (hayupo pichani) alijishindia tikect ya Ndege ya kuelekea
Doha.
Balozi Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Al-Maadadi.
Katibu Mkuu Balozi Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi waliohudhuria maadhimisho hayo.
Picha na Reginald Philip
No comments:
Post a Comment