Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu,Mkoani Manyara,Hudson
Stanlay Kamoga,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani)
kuhusiana na mikakati aliyojiwekea katika utendaji wake wa kazi kwa
watumishi wa halmashauri hiyo..Picha na Mary Margwe.
Na Mary Margwe, Mbulu
.Ndoto yake ni kuibadilisha Mbulu kuwa nchi ya vitunguu swaumu.(Mbulu the land of garlic).Asisitiza mambo muhimu matatu ya kuleta mabadiliko ya maendeleo yanayotokana na neno P I A
P---Patriotism---Uzalendo
I----Integrity. ----Uadirifu na
A---Accountabiliyt---Uwajibikaji
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini,Mkoani Manyara ,
Hudson Stanley Kamoga, amewataka watendaji,madiwani na wananchi kwa
ujumla kumpa ushirikiano katika utendaji wake wa kazi ya kuwatumikia
wananchi Wilayani humo kwa lengo la kusukuma gurudumu la maendeleo.
Akiongea
na waandishi wa habari Jana ofisini kwake, Kamoga alisema ushirikiano
katika nyanja yoyote ile inahitajika ili kufikia malengo,hivyo naye
anaomba apewe ushirikiano ili kuweza kufikia malengo aliyojiwekea katika
kuhakikisha Mbulu unajua na maendeleo ya kweli na si vinginevyo.
Kamoga
alisema ushirikiano huo uende sambamba na kuwataka wakuu wa idara kumpa
mpango kazi wake wa mwezi mmoja kuwa mini amefanya kwenye idara yake,
kama idara wamekutana na vikwazo / changamoto gani na ni kwa namna gani
wamejipanga kukabiliana na changamoto hizo
Kamoga
alisema yeye kama Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mbulu,
angependa kuona madiwani na watendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo
wakiwa wanazungumza lugha moja tu ya maendeleo na si vinginevyo.
"Lazima
kama Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu,nihakikishe
watendaji na madiwani wanafanya kazi kama timu moja, kwani siku zote
umoja ndio hujenga kitu chochote cha maendeleo na msingi wa maendeleo ni
ushirikiano yaani umoja,hivyo uwezo ninao wa kulisimamia hili na
hatimaye kuweza kuona tuko wapi, tumetoka wapi na tunatarajia kwenda
wapi " alisema Kamoga.
Aidha
alisema ili kufikia malengo aliyojiwekea kikamilifu, ametengeneza
utaratibu ambapo angependa watendaji wake wote wa halmashauri waufuate
na kuuzingatia kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya Kila
siku.
"Wanahabari
kuna hili neno lenye herufi tatu tu lakini lina maana kubwa sana katika
utekelezaji wa majikumu yetu ya Kila siku ambapo tukilishika kikamilifu
hakuna kitakachokwenda mrama,ambalo linasomeka P I A , P ...limesimama
kama neno Patriotism (Uzalendo) , herufi ya pili ni I...limesimama kama
Integrity (uadirifu) na la tatu ni A...ambalo limesimama kama
Accountability (Uwajibikaji).
Kamoga
alifafanua kua kufuatia maana ya neo PIA, anataka kutengeneza
halmashauri yenye watendaji wazalendo, na hao wazalendo lazima wabebe
uadirifu kisha tatu Uawajibikaji ,hawa wazalendo ambayo ni waadirifu
lazima wawe waajibikaji ,ambapo alisema kukishakua hivyo katika Kila
idara zote ambazo watendaji wake wako hivyo, halmashauri hiyo itapiga
hatua kubwa mbele kimaendeleo katika kukabiliana na changamoto zilizopo.
" Kwa
hiyo wote tuibebe neno P I A ili tuwe wazalendo, waadirifu na pia tuwe
waajibikaji Kila mmoja ahakikishe ana anawajibika kwenye nafasi yake wa
uwezo wake wote ,hapo tutasonga hatua mbele kimaendeleo,hii ndio misingi
yangu ninayotaka tujijengee na watendaji wangu wa halmashauri
Je? Ni Mikakati gani ambayo itamwezesha Kamoga kufikia malengo yake?
Kila
mmoja atahakikisha anafanya kazi kwa mazingira yake bila kuingiliana na
mwingine,ambapo ana amini madiwani kwa moyo na uchu walionao wa kutaka
maendeleo katika jamii hususani ndani ya kata zao.
Aidha
alisema kubwa madiwani watashirikiana kwa umakini kabisa na watendaji
walipo kwenye kata hadi ngazi ya vitongoji vyao, ili kuhakikisha
wanapunguza migogoro iliyopo vijijini na kwenye kata zao katika kuleta
maendeleo ndani ya kata na vijiji, " Lakini pia watendaji wangu wafanye
kazi kwa uzalendo, uadirifu na Uwajibikaji wa hali ya juu, hii ndiyo
mikakati yangu .
Pamoja na hayo yote lakini je? Nini Ndoto zake za baadaye kwa Halmashauri ya Wilaya hiyo kama Mkurugenzi??
"Ndoto
yangu kubwa nataka na natamani kuona watu wa ndani na nje ya nchi yaani
Tanzani na duniani kote ijue kuwa Mbulu ionekane kama nchi ya vitunguu
swaumu ( The land of Garlic) kule Bashay na Mbulu kiujumla tunazalisha
vitunguu bora huku wananchi wake bado wanaonekana kutonufaishwa na zao
hili" alisema Kamoga.
Alifafanua
kuwa lengo vile vitunguu vibadilike kubadilisha maisha wana Bashay
,wakulima wafurahie uwepo wa uzalishaji mkubwa wa vitunguu swaumu,ambapo
alibainisha vitunguu vinavyosafirishwa kwenda nje ni vema viende
vikishakua vimewekwa lebo kuonyesha hili ni zao la MBULU ( this is the
product of Mbulu / Mbulu product) .
"Hiki
ndicho natamani sana sana ,kwa hiyo mtu anakula kitunguu swaumu akiwa
anajua kabisa kuwa anakula kitunguu cha wapi , mtu yoyote akienda sokoni
moja kwa moja aulize nataka kitunguu cha Mbulu, huu ndio ufahari
wangu,nitasimamia kuhakikisha hili linatekelezeka" alisema Kamoga.
No comments:
Post a Comment