Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango (aliyevaa nguo nyeusi) akiangalia na kupata maelezo kutoka kwa
Injinia wa kituo Bw. Rajabu Kindunda (wa tatu kulia) kuhusu Bwawa la
Kidatu ambalo maji hukusanywa kutoka mto Rufiji kabla ya kutumika kwa
ajili ya kuzalisha umeme. Wengine pamoja nae ni wataalamu kutoka Tume ya
Mipango na TANESCO.
Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango (aliyevaa nguo nyeusi) akiangalia eneo la mradi wa kuzalisha
umeme Kidatu na kupata maelezo kuhusu faida na changamoto za mradi
kutoka kwa Injinia wa TANESCO kituo cha Kidatu Bw. Rajabu Kindunda (wa
tatu kulia). Wengine ni wataalamu kutoka Tume ya Mipango na TANESCO.
Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango (aliyekaa) akipata maelezo kuhusu namna Kituo cha Kihansi
kinavyofanyakazi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambayo imeboresha
utendaji kazi kwa wafanyakazi na mitambo ambayo inatumika kuzalisha
nishati ya umeme.
Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango (aliyevaa nguo nyeusi) pamoja na maofisa kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa Injinia kituo cha Kidatu Bw.
Yonah Mwasajone (wa kwanza kushoto) kuhusu Sub Station ambayo baada ya
umeme kuzalishwa katika mitambo ya kufua umeme Kidatu hutumika
kuuingiza katika Grid ya Taifa.
Na: Thomas Nyindo
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
No comments:
Post a Comment