Matukio : Mapipa yenye Pombe Haramu aina ya Gongo Yamwagwa Kuzuia Kipindupindu, Jijini Arusha - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 31 December 2015

Matukio : Mapipa yenye Pombe Haramu aina ya Gongo Yamwagwa Kuzuia Kipindupindu, Jijini Arusha

Mgambo wa jiji Wakimwaga pombe za kienyeji aina ya Gongo zilizokutwa kwenye nyumba za wakazi wa Mtaa wa Matejo jijini  Arusha katika operesheni ya tokomeza kipindupindu iliyofanywa na Halmashauri kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa,kufuatia mazingira machafu na hatarishi ya uandaaji wa pombe hizo,mitaa hiyo ni maarufu kwa uuzaji wa pombe za kienyeji.
Mgambo wa jiji akimwaga pombe za kienyeji aina ya Gongo zilizokutwa kwenye nyumba za wakazi wa Mtaa wa Matejo jijini  Arusha katika operesheni ya tokomeza kipindupindu iliyofanywa na Halmashauri kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa,kufuatia mazingira machafu na hatarishi ya uandaaji wa pombe hizo,mitaa hiyo ni maarufu kwa uuzaji wa pombe za kienyeji.
Mgambo wa jiji akimwaga pombe za kienyeji aina ya Gongo zilizokutwa kwenye nyumba za wakazi wa Mtaa wa Matejo jijini  Arusha katika operesheni ya tokomeza kipindupindu iliyofanywa na Halmashauri kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa,kufuatia mazingira machafu na hatarishi ya uandaaji wa pombe hizo,mitaa hiyo ni maarufu kwa uuzaji wa pombe za kienyeji. Picha na Ferdinand Shayo

Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog,Arusha.

Wananchi wa Mtaa wa Matejo uliopo jijini Arusha wameiomba serikali iwapatie mikopo ili waweze kufanya shughuli mbadala za kujiingizia kipato badala kujishughulisha na uuzaji wa pombe haramu ambazo zinadaiwa kuwa sababu mojawapo ya kuenea kwa ugonjwa wa kipindu pindu kutokana na mazingira machafu na hatarishi ya uandaaji wake.

Wananchi hao wakizungumza katika operesheni  ya tokomeza kipindupindu iliyoendeshwa na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ,kwa kushirikiana na Halmashauri na kamati ya Ulinzi na usalama wameteketeza mitambo ya kupikia pombe hizo aina ya piwa,dadi na chang`aa  ambazo pia huathiri afya za watu.

Ester Stephano Shaka  ambaye ni Muuzaji wa pombe hizo na Wilfred Lyakimu na walisema kuwa maisha yao yanategemea biashara ya pombe za kienyeji ambazo huwasaidia kusomesha watoto na kupata mahitaji ya nyumbani hivyo ameiomba serikali iwapatie mikopo ili waweze kufanya biashara mbadala badala ya kutumia nguvu kutokomeza biashara hiyo.

“Tunategemea shughuli ya kupika na kuuza pombe za kienyeji kuendesha maisha yetu ,serikali haiwezi kuwaajiri watu wote tunaiomba serikali itutafutie shughuli mbadala kwani hapa ndio tunapata chakula na mahitaji muhimu “ Alisema Wilfred

Mkazi wa Matejo Jovan George alisema kuwa kutokana na tatizo la ajira limewapelekea watu wengi kujiingiza katika biashara hiyo na matumizi ya pombe hivyo ameitaka serikali kutafuta njia mbadala .

Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira jiji la Arusha  ,James Lobikoki alisema kuwa uteketezaji wa pombe haramu ni moja kati ya jitihada wanazozifanya katika  utekelezaji wa operesheni tokomeza kwani kutokana na mazingira machafu ya uandaaji wa pombe hizo kwani zoezi hilo ni endelevu.

Alisema Ugonjwa wa kipindupindu umeenea katika maeneo mengi nchini tayari wananchi wameanza kuchukua tahadhari ya kuweka mazingira safi licha ya baadhi ya maeneo kukithiri  kwa uchafu hivyo kukwamisha jitihada za kutokomeza ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment