Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk. Ally Yahaya SIMBA
1. Katika shughuili zake za udhibiti wa huduma
za mawasiliano nchini, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imepokea malalamiko
kutoka kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano dhidi ya kuwepo mazingira yasiyo
salama katika huduma za mawasiliano na hivyo kusababisha kufanyika kwa vitendo
vya utapeli unaofanywa kwa kutuma jumbe za udanganyifu na kulaghai, hivyo kusababisha
watu kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu. Kwa mfano kupokea ujumbe kutoka
namba unayoifahamu ukikuagiza utume fedha au ujumbe wa kashfa au matusi wakati
hautoki kwa mhusika mwenye namba. Mamlaka imepokea malalamiko mengi kutoka kwa
wateja na malalamiko mengine hupelekwa Polisi. Kwa miezi miwili tu, matukio 42
yameripotiwa Polisi pamoja na TCRA ambayo tukio moja tu linakuwa na ulaghai wa
takribani milioni 25 peke yake.
2. Tarehe 16 Oktoba, 2015 Mamlaka iliwakumbusha
watoa huduma za simu nchini juu ya wajibu wao kuchukua hatua za kusheria na
kitaalamu ili kulinda watumiaji dhidi ya utumaji wa jumbe za kilaghai na
kuchukua hatua mara moja kuzuia mitandao yao kutumika kutuma jumbe za
udanganyifu na kulaghai. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mamlaka tarehe
16 Desemba, 2015 Mamlaka ilibaini kuwa
kampuni za Benson Informatics Limited (inayojulikana kama Smart), MIC
Tanzania Limited (inayojulikana kama Tigo), Airtel Tanzania Limited, Viettel
Tanzania Limited (inayojulikana kama Halotel) and Zanzibar Telecom Limited inayojulikana
kama Zantel) zimeshindwa, zimepuuzia na zimekataa kufuata maagizo ya Mamlaka
kuchukua hatua mara moja kuzuia mitandao yao kutumika kutuma jumbe za kilaghai
kinyume na Kanuni Na.8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya
mwaka 2011 [the Electronic and Postal Communications (Computer Emergency
Response Team) Regulations, 2011].
3.
Tarehe 18 Disemba, 2015 Mamlaka iliwaamuru
watoa huduma za mawasiliano waliotajwa hapo juu kufika mbele ya Mamlaka na
kujieleza kwa nini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yao kwa kuvunja sheria
na kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielectroniki na Postal ya Mwaka 2011
[the Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team)
Regulations, 2011] kwa kushindwa kuweka mazingira salama kwa watumiaji wa
huduma za mawasiliano.
4.
Watoa huduma walifika na kutoa maelezo ya utetezi
kati ya tarehe 21 na 23 Desemba, 2015.
5. Baada ya kuwasikiliza na kutilia maanani
utetezi wa watoa huduma na kwa mujibu wa uchunguzi na majaribio uliofanywa na
Mamlaka, Mamlaka imejiridhisha kuwa mitandao ya watoa huduma waliotajwa hapo
juu haikuwa salama na kuwa watoa huduma hao walishindwa kufuata maelekezo ya
Mamlaka juu ya kuweka mazingira salama katika huduma wanazotoa. Hivyo Mamlaka
imejiridhisha kuwa watoa huduma wamekiuka matakwa ya Kanuni ya 8(a) ya Kanuni
za Mawasiliano ya Kielectroniki na Postal ya mwaka 2011 (The Electronic and
Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011) inayowataka
watoa huduma kuweka mazingira ya mitandao salama kwa kuchukua hatua za kusheria
na kitaalamu ili kulinda watumiaji dhidi ya uhalifu ikiwa ni pamoja na utumaji
wa jumbe za kilaghai kupitia mitandao yao.
6. Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 cha Jedwali la Pili
katika Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sura ya 306 ya Sheria
za Nchi, kinachoipa Mamlaka uwezo wa kutoa adhabu kwa Wenye Leseni dhidi ya
uvunjifu wa Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni, Mamlaka ya Mawasiliano imetoa:
A.
Onyo kali kwa Kampuni za:
(i)
Benson Informatics Limited (inayojulikana
kama Smart),
(ii)
MIC
Tanzania Limited (inayojulikana kama Tigo),
(iii)
Airtel Tanzania Limited,
(iv)
Viettel Tanzania Limited (inayojulikana kama Halotel),
na
(v)
Zanzibar Telecom Limited (inayojulikana kama
Zantel).
kwa
kushindwa kutimiza matakwa ya Kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki
na Postal ya mwaka 2011 [the Electronic
and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011]
kwa kushindwa kuweza mazingira salama kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano.
B.
Imeamuru Kila Kampuni husika:
(i) Kuhakikisha
kuwa, kuanzia siku ya kutolewa kwa amri hii, inaweka mazingira salama katika
mtandao wake yatakayozuia utumaji wa jumbe za kilaghai (yaani ‘spoofed messages’)
na matishio mengine ya kiusalama;
(ii) Kulipa faini ya Shilingi za Kitanzania
Milioni Ishirini na Tano (Shs 25,000,000.00) kwa Mamlaka ya Mawasiliano kabla
ya tarehe 29 Januari, 2016; na
(iii) Endapo
Makamuni haya yatashindwa kutimiza amri Na.2 hapo juu, Mamlaka itachukua hatua
zaidi za kisheria na kiudhibiti dhidi ya Kampuni ya Simu husika.
7.
Aidha, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapeda
kuchukua fursa hii kuwatahadharisha wananchi kuwa makini na jumbe za kuwataka kutuma
fedha bila ya kuwa na uhakika. Inashauriwa kuhakiki ujumbe husika kwa kupiga
simu na kuongea na mhusika kabla ya kufanya maamuzi ya kutuma fedha hata kama
namba inayotumika unaijua. Vilevile wawe makini wanapopokea jumbe zinazoonesha
zinatoka kwa mtu fulani wanayemjua kumbe ni matapeli wanaotumia ulaghai kwa
njia hii ya “spoofing”.
IMETOLEWA NA
………………………………………….
Dkt.
Ally Y. Simba
MKURUGENZI
MKUU
No comments:
Post a Comment