Picha zote na Fatma Salum (MAELEZO)
SERIKALI imeboresha matumizi ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielekitroniki katika mamlaka za serikali za mitaa.
Hayo
yamesemwa na msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na
Serikali za mitaa (TAMISEMI) Bi. Rebecca Kwandu leo jijini Dar es
salaam.
Bi
Rebecca amesema kuwa TAMISEMI imekuwa ikiendelea kwa nyakati tofauti
kufanya maboresho mbalimbali ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii
na kuzisaidia mamlaka hizo katika kuongeza mapato ya ndani na kuondokana
na uteuzi wa ruzuku kutoka Serikali Kuu.
“Ofisi
ya Waziri Mkuu –TAMISEMI iliamua kuanzisha mfuko wa Local Governement
Collection Information System (LGRCIS) baada ya kufanya tafiti
mbalimbali kwa nyakati tofauti na zilionyesha kuwa hakukuwa na mfumo
wowote wa kielektroniki kurahisisha ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya
Halmashauri” alifafanua Bi. Rebecca.
Mbali
na hayo Msemaji huyo alisema kuwa miongoni mwa malengo makuu ya
kuanzishwa kwa mfumo wa LGRCIS ni pamoja na kupata taarifa za walipa
kodi wa mamlaka za serikali za mitaa na kuhifadhiwa kwa usahihi katika
kanzi data ya mfumo.
“
Kupata takwimu sahihi ya vyanzo vya mapato na kufanya usuluhishi kati
ya kilichokusanywa na kilichotarajiwa kukusanywa, kuongeza mapato kwa
kasi zaidi kwa kuwa na uhakika wa makusanyo katika vyanzo vikuu, kuweka
uwazi na uwajibikija katika makusanyo ya mapato,na kuhimarisha ulipaji
miamala ya kodi na tozo itakayofanywa na walipakodi” aliongeza Bi
Rebecca.
Pia
alisema kuwa matarajio ya TAMISEMI ni kuwa mfumo wa LGRCIS utaleta
mabadiliko makubwa katika Halmashaurina kuachana na utegemezi wa ruzuku
kutoka Serikali kuu.
Hata
hivyo teknolojia pekee ya matumizi ya TEHAMA haiwezi kuleta mabadiliko
pasipo fikra za watumiaji wa mfumo wa walipakodi kubadili mazoea.
No comments:
Post a Comment