
Wakuu
wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika kikao hicho,kutoka
kuslia ni Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka, Helman Kapufi (Mkuu wa
wilaya ya Same) Novautus Makunga (Mkuu wa wilaya ya Moshi) na Lembris
Kipuyo (Mkuu wa wilaya ya Rombo).

Baadhi ya wakurugenzi wakiwa katika kikao hicho.


Watendaji wengine wa serikali wakifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro alipokutana nao .


Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro,Severine Kahitwa akizungumza katika kikao hicho.

Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kilimanjaro.

Baadhi
ya watendaji wa taasisi za umma,kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya
maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,Joyce Msiru.

Badhi ya watumishi katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
Na Dixon Busagaga wa kanda ya kaskazini.
KATIKA
kutekeleza kauli mbiu ya Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,John Magufuli ya “Hapa Kazi tu” Serikali mkoani Kilimanjaro
imetangaza kusitisha likizo na ruhusa zote kwa watumishi wake katika
kipindi cha siku kuu za Krismasi na mwaka mpya.
Agizo
hilo linakuja wakati tayari baadhi ya watumishi wa Serikali kuanza
taratibu za kuomba likizo na ruhusa kwa ajili ya kwenda kushiriki siku
kuu za mwisho wa mwaka za Krismasi na mwaka mpya.
Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makala alitangaza uamuzi huo jana wakati wa
kikao cha kazi alichoitisha na wakuu wa wilaya zote za mkoa,
wakurugenzi, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na watendaji wengine wa
serikali.
“Mh
Rais ametoka kwenye kampeni hajapumzika,Makamau wa rais ametoka kwenye
kampeni hajapumzika ,Waziri mkuu pia vivyo hivyo sasa sisi ni nani
twende kwenye mapumziko ya siku kuu ya Krismasi.”alihoji Makala.
“Kwa
maana hiyo ili haya tunayotaka ya elimu bure ,kukabiliana na
Kipindupindu ,kwa madaraka niliyopewa kama mkuu wa mkoa nasitisha likizo
zote,kwa Wakuu wa wilaya ,Wakurugenzi na wakuu wote wa idara ili mambo
haya yaweze kutekelezwa,tumesema Hapa ni kazi tu”aliongeza Makala.
Alisema
utekelezaji wa agizo la rais la kufanya usafi siku ya sikuu ya Uhuru
inayofanyika Desemba 9 kila mwaka ,mapambano ya ugonjwa hatari wa
Kipindupindu ambao umeendelea kusambaa sehemu kubwa ya nchi hayawezi
kusubiri hadi watusmishi wa serikali watoke likizo.
No comments:
Post a Comment