Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kulia) akitoa neno la ukaribisho kwa wadau wa sekta ya elimu wakati wa hafla ya kukabidhi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Katikati ni mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa aliyemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome. Kushoto ni Ofisa wa Ubalozi wa China, LIU Yun.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),
limekabidhi rasmi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo
vya ualimu nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Makabidhiano
hayo yamefanyika jana jijini Dar es salaam katika hafla iliyohudhuriwa
na wadau walioshiriki katika uandazi wa kitabu hicho, ikiwamo serikali
ya China.
Kitabu
hicho ni matokea ya mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wenye
lengo la kusaidia Serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi
na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.
Mradi
huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa
ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.
Mgeni
rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa akisoma hotuba
ya ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Prof. Sifuni Mchome wakati wa hafla ya kukabidhiwa kitabu cha
mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini kwa ajili ya
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kilichoandaliwa na mradi wa CFIT
wa UNESCO na serikali ya China.
Akipokea
kitabu hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Prof. Sifuni Mchome, Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella
Bhalalusesa ameishukuru UNESCO na serikali ya China ya kuwezesha
upitiaji wa kitabu hicho kinachotoa mwelekeo wa mafunzo ili kuambatana
na maagizo ya viwango yaliyotolewa na Shirika la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO).
Alisema kitabu hicho kinatoa mwelekeo wa utekelezaji wa elimu ya Tehama kwa kuzingatia uwezo na weledi katika ufundishaji.
Kamishina
huyo amesema kwamba kazi ya kuangalia viwango hivyo iliyofanywa
kutokana na Mfuko wa China na Unesco kwenye moduli sita za uelewa na
elimu ya teknolojia kwenye Tehama.
Alishukuru
timu iliyopitia viwango hivyo na kusema serikali ya Tanzania inashukuru
msaada huo wa Unesco na serikali ya China kwa kufanikisha kazi hiyo kwa
ufanisi mkubwa.
Ofisa
wa Ubalozi wa China, LIU Yun akitoa salamu za Balozi wa China nchini
kwenye hafla ya kukabidhi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa
vyuo vya ualimu na walimu nchini kwa ajili ya Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi.
Ni
matumaini yake kwamba sasa Tanzania ina kielelezo cha kufuatia katika
kufanikisha maandalizi ya walimu wenye weledi na uwezo katika kufundisha
na kutumia teknolojia ya Tehama.
Naye
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues akizungumza kabla ya kukabidhi kitabu hicho alisema UNESCO
itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuimarisha elimu
ya Tehama ili kufungua njia pana zaidi ya maendeleo.
Aidha
ameikumbusha serikali ya Tanzania kutumia vyema kitabu hicho katika
kuhakikisha kwamba mafunzo ya kariba ya hali ya juu yanatolewa ili kuwa
na mafanikio makubwa katika sekta zote za elimu na teknolojia.
Alisema
kitabu hicho kinatoa mwelekeo wa hatua kwa hatua katika mafunzo ya
Tehama na namna ya kufanikisha katika kumwelimisha mwanafunzi na vitu
vinavyoweza kufanywa ili kuhakikisha kwamba elimu sahihi inawafikia
wahusika.
Naye
Balozi wa China nchini, Dk. Lu Youqing kupitia kwa Ofisa wa Ubalozi Liu
Yun aliyefika kwenye hafla hiyo, alisema kwamba serikali ya China
itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha elimu ya Tehama
nchini.
Naye
Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT Kutoka UNESCO, Faith Shayo
alishawahi kusikika akisema utoaji wa mwongozo huo ni sehemu ya
maandalizi ya mafunzo na matumizi ya maabara katika vyuo vya Monduli na
Tabora katika kufunza Tehama ili kuboresha mafunzo na ufundishaji.
Ingawa
kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora
na Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu
ambavyo vitaingizwa katika mradi.
Mratibu
wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo akielezea
maandalizi na hatua walizopitia katika uandaaji wa kitabu hicho mpaka
kukamilika kwa wadau wa sekta ya elimu walioshiriki hafla hiyo.
Meza kuu ikimpongeza Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo (hayupo pichani).
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues (kulia) akimkabidhi Kamishna wa Elimu, Prof.Eustella
Bhalalusesa kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya
ualimu na walimu kilichoandaliwa na mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali
ya China. Mradi huo una lengo la kusaidia serikali ya Tanzania
kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama
na kuitumia.
Mgeni
rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa (walioketi
kushoto) na Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues katika picha ya pamoja na timu iliyoshiriki kuandaa kitabu cha
mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu
kilichoandaliwa na mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wakati
hafla ya makabidhiano ya kitabu hicho iliyofanyika katika hoteli ya
Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Mradi huo una lengo la kusaidia
serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa
kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.
Pichani
juu na chini baadhi ya wadau wa sekta ya elimu na maafisa wa Shirika la
UNESCO waliohudhuria halfa ya makabidhiano ya mwongozo wa mafunzo ya
Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini kwa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye hoteli
ya Protea Courtyard.
Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues akijadiliana jambo na Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT
kutoka UNESCO, Faith Shayo Kulia aliyeketi ni Kaimu Katibu Mtendaji wa
Tume ya Taifa ya UNESCO, Dr. Moshi Kimizi.
Mgeni
rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa katika picha ya
pamoja na wadau wa sekta ya Elimu nchini mara baada kupokea kitabu cha
mwongozo wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu
kilichoandaliwa na mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wakati
hafla ya makabidhiano ya kitabu hicho kilichokabidhiwa kwa Kamishna wa
Elimu nchini katika hoteli ya Protea Courtyard Hotel jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment