Baadhi
ya waandishi wa vyombo vya habari mbalimbali nchini wakiwa kwenye hafla
fupi ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni
4.9 kwa timu zote zinazoshiriki ligi kuu ya mpira wa miguu ya Vodacom
Tanzania bara(VPL)leo vilivyokabidhiwa na mdhamini mkuu wa ligi hiyo
kampuni ya Vodacom Tanzania.
Mkuu
wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa akiongea na
waandishi wa habari na wawakilishi wa vilabu mbalimbali wa timu
zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,wakati wa hafla fupi ya
kukabidhiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 4.9 kwa
timu zote zinazoshiriki ligi hiyo leo vilivyokabidhiwa na mdhamini mkuu
wa ligi kampuni ya Vodacom Tanzania,kushoto ni Meneja Masoko wa
shirikisho la mpira wa miguu Tanzania,(TFF)Peter Simon.
Vijana
wakitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini za timu ya African
Sport ya Tanga na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni
4.9 kwa msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016
zilizokabidhiwa rasmi leo na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya
Vodacom Tanzania.
Wanamitindo
wakipita kuitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini za timu ya
Majimaji na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa
msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016 zilizokabidhiwa
rasmi leo na mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, Boniface
Wambura(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania,Kelvin Twissa(watano toka kushoto)akiwa kwenye picha na
mwakilishi wa timu ya Azam FC pamoja na wanamitindo waliokuwa
wakiitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini na vifaa mbalimbali
vya timu ya Azam FC vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya
msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016.Vifaa hivyo
vilikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na mdhamini mkuu wa ligi hiyo
kampuni ya Vodacom Tanzania.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, Boniface
Wambura(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania,Kelvin Twissa(watano toka kushoto)akiwa kwenye picha na
mwakilishi wa timu ya Coastal Union pamoja na wanamitindo waliokuwa
wakiitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini na vifaa mbalimbali
vya timu hiyo vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya msimu
mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016.Vifaa hivyo
vilikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na mdhamini mkuu wa ligi hiyo
kampuni ya Vodacom Tanzania.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania,Boniface
Wambura(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania,Kelvin Twissa(watano toka kushoto)akiwa kwenye picha na
mwakilishi wa timu ya Mbeya FC pamoja na wanamitindo waliokuwa
wakiitambulisha jezi mpya za nyumbani na ugenini na vifaa mbalimbali
vya timu hiyo vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya msimu
mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016.Vifaa hivyo
vilikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na mdhamini mkuu wa ligi hiyo
kampuni ya Vodacom Tanzania.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania,Boniface
Wambura(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania,Kelvin Twissa(watano toka kushoto)akiwa kwenye picha na
mwakilishi wa timu ya Yanga sports club ya jangwani jijini Dar es salaam
pamoja na wanamitindo waliokuwa wakiitambulisha jezi mpya za nyumbani
na ugenini na vifaa mbalimbali vya timu hiyo vyenye thamani ya shilingi
Milioni 4.9 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara 2015/2016.Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na
mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania,Boniface Wambura
na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa
wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanamitindo waliokuwa wakizitangaza
jezi mpya za timu 16 zitakazoshiriki katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara 2015/2016 wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa jezi hizo na vifaa
mbalimbali vyenye thamni ya zaidi ya shilingi milioni 4.9 na mdhamini
mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania kwa timu zote
zitakazoshiriki katika ligi hiyo.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania,Boniface
Wambura(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania,Kelvin Twissa(watano toka kushoto)akiwa kwenye picha na
mwakilishi wa timu ya Simba Sports Club ya Msimbazi jijini Dar es Salaam
pamoja na wanamitindo waliokuwa wakiitambulisha jezi mpya za nyumbani
na ugenini na vifaa mbalimbali vya timu hiyo vyenye thamani ya shilingi
Milioni 4.9 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara 2015/2016.Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na
mdhamini mkuu wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.
KAMPUNI
ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ambayo ni mdhamini mkuu wa Ligi kuu
ya mpira wa miguu Tanzania bara leo imekabidhi vifaa kwa timu
zinazoshiriki ligi hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni 490,000,000/=
Akikabidhi
vifaa hivyo leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na
Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa,alisema kuwa kwa mara nyingine
tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom
inakabidhi vifaa mbalimbali vya ligi ambavyo ni jezi mbalimbali, viatu
vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda ugoko, nguo za mazoezi, nguo za
kawaida, gloves na vifaa vingine vingi vinavyohitajika.
“Tunajisikia
furaha kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwa tunatekeleza matakwa
ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki ligi
zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya wa ligi wa 2015/2016”Alisema
Twissa.
Twissa
alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo
unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda
kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata burudani ya
mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa
duniani kote,ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na
taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka katika sekta hii.
Aliwataka
wadhamini wengine kujitokeza ili kuboresha zaidi ligi ya Tanzania na
kuongeza maslahi kwa wachezaji wanaoshiriki katika ligi “Tukiunganisha
nguvu timu zetu zinaweza kuwa na wachezaji wa kimataifa pia ni muhimu
kwa wadau mbalimbali kuanza kuwekeza katika timu za vijana chipukizi kwa
kuwa vipaji vinaanzia ngazi ya chini ambako vinapaswa kuibuliwa na
kuendelezwa ”Alisema Twissa.
Naye
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi,Boniface Wambura aliishukuru
Kampuni ya Vodacom, na kuvitaka vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya
Vodacom kuheshimu chapa ya mdhamini wakati wote wa mechi za ligi.
“Ninatoa
mwito kwa vilabu vyote kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini katika
kuhakikisha ligi inafanikiwa kama inavyotakiwa,”alisema.
Aliongeza
kuwa TFF isingependa kutumia kanuni na sheria kuadhibu klabu
inayokwenda kinyume, bali kila klabu izingatie masharti ya mdhamini
kama ambavyo anavyotimiza haki yake ya kuwapatia vifaa.
Alisema
ligi ya mwaka huu itakuwa bora kutokana na maandalizi yote kukamilika
mapema pia timu zitazoshiriki zimeziandaa vya kutosha kuhakikisha ligi
inakuwa na msisimko na ushindani mkubwa.
No comments:
Post a Comment