Baadhi
ya Maafisa Waandamizi, Wakaguzi, Wakaguzi Wasaidizi, Stesheni Sajini,
Sajini na Koplo wa Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi na Usalama wakifuatilia
masuala mbalimbali wakati hafla ya utoaji wa nishani ya utumishi
uliotukuka Tanzania, nishati ya utumishi wa muda mrefu na nishani ya
utumishi wa muda mrefu na tabia iliyofanyika jana (Jumanne Septemba 1,
2015) Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Asha-Rose Migiro (kulia) akifuatilia masuala
mbalimbali wakati hafla ya utoaji wa nishani ya utumishi uliotukuka
Tanzania, nishati ya utumishi wa muda mrefu na nishani ya utumishi wa
muda mrefu na tabia iliyofanyika jana (Jumanne Septemba 1, 2015) Ikulu
Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maimuna
Tarishi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante
Ole Gabriel (kulia) akifuatilia masuala mbalimbali wakati hafla ya
utoaji wa nishani ya utumishi uliotukuka Tanzania, nishati ya utumishi
wa muda mrefu na nishani ya utumishi wa muda mrefu na tabia iliyofanyika
jana (Jumanne Septemba 1, 2015) Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania, Jenerali Adolf
Mwamunyange (kushoto), Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest
Mangu na Kamishna Jerenali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Minja
wakisoma ratiba ya hafla ya utoaji wa nishani ya utumishi uliotukuka
Tanzania, nishati ya utumishi wa muda mrefu na nishani ya utumishi wa
muda mrefu na tabia iliyofanyika jana (Jumanne Septemba 1, 2015) Ikulu
Jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu msaafu Joseph
Warioba wakisoma ratiba ya hafla ya utoaji wa nishani ya utumishi
uliotukuka Tanzania, nishati ya utumishi wa muda mrefu na nishani ya
utumishi wa muda mrefu na tabia iliyofanyika jana (Jumanne Septemba 1,
2015) Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akimtunuku ACP Vincent Mosses Karata nishani ya
utumishi wa muda mrefu Tanzania katika hafla iliyofanyika ikulu Jijini
Dar Es Salaam jana( Jumanne Septemba 1, 2015).
Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Dkt. Jakaya Kikwete
akimtunuku Brigedia Jenerali Jacob Gideon Kingu nishani ya utumishi
uliotukuka Tanzania katika hafla iliyofanyika ikulu Jijini Dar Es Salaam
jana( Jumanne Septemba 1, 2015).
Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Dkt. Jakaya Kikwete
akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa majeshi ya vikosi vya Ulinzi na
Usalama mara baada ya hafla ya utoaji wa nishani kwa Maafisa
Waandamizi, Wakaguzi, Wakaguzi Wasaidizi, Stesheni Sajini, Sajini na
Koplo wa Vikosi vya Majeshi ya Ulinzi na Usalama wakati wa hafla ya
utoaji wa nishani ya utumishi uliotukuka Tanzania, nishati ya utumishi
wa muda mrefu na nishani ya utumishi wa muda mrefu na tabia iliyofanyika
jana (Jumanne Septemba 1, 2015) Ikulu Jijini Dar es Salaam.
1 Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Dkt. Jakaya Kikwete
akimtunuku ACP Bakari Namkaa Ndembo nishani ya utumishi mrefu Tanzania
katika hafla iliyofanyika jana jumanne (Septemba 1, 2015) Ikulu Jijini
Dar es Salaam.
Na
Lilian Lundo
MAELEZO
Dar
Es Salaam
Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete amewatunuku nishani ya utumishi uliotukuka, utumishi mrefu na tabia Njema
maofisa wa majeshi mbalimbali 30.
Kati ya maofisa hao 10
ni kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), 10 kutoka Jeshi la
Polisi na 10 wengine wanatoka Jeshi la Magereza.
Akiwataja maofisa waliopata nishani za utumishi
uliotukuka, Mkurugenzi wa shughuli za Ikulu Juluus Magore alisema nishani hiyo
hutunukiwa kwa maofisa walio hai wa cheo cha Meja kwenda juu kwa JWTZ na kwa
Polisi hutolewa kwa Mrakibu au maofisa waandamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa
waliotimiza si chini ya miaka 20.
Waliotunukiwa nishani
hiyo ni Meja Jenerali Yacub Hassan Mohamed, Brigedia Jenerali Jacob Gideon
Kingu, Kanali Fadhil Omary Nondo, Luteni Kanali Ian Alphonce Haule, Kamishina wa
Polisi Elice Angelo Mapunda, Naibu Kamishna wa Polisi Samson Manoc Kassala,
Naibu Kamishna wa Polisi Rashid Ally Omary, Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed
Ramadhan Mpinga.
Wengine ni pamoja na Kamishna
wa Magereza Gaston Kalamu Sanga, Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Magereza Gideon
Marco Nkana, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Augustine Sangalali Mboje
na Kamishna Msaidizi Muandamizi wa MagerezaVenant Jacob Kayombo.
Aidha Magore alisema
nishani ya utumishi mrefu hutunukiwa kwa maofisa walio kwenye utumishi hai
wenye kamisheni wa JWTZ na maofisa waliotangazwa gazetini wa Polisi, Magereza
na Idara ya Usalama wa Taifa waliotimiza utumishi wa miaka isiyopungua 15
wakiwa wenye tabia njema ya kuweza kusifiwa.
Aliwataja maofisa
waliotunukiwa nishani hiyo kuwa ni Kanali Mary Bayu Hiki, Kanali Msafiri Mtalika
Hamis, Meja Bernard Paul Masala Mlunga, Kamishna wa Polisi Valentino Longino Mlowol,
Naibu Kamishina wa Polisi Ally KihuriLugendo.
Wengine ni Kamishina Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi Mboje John Kanga , Kamishna Msaidizi wa Magereza Vincent
Protas Marissa, Kamishina Msaidizi wa Magereza Bakari Namkaa Ndembo na Kamishina
Msaidizi .
Msaidizi wa Magereza Vincent Moses Karata
Aidha alisema nishani
ya utumishi mrefu na tabia njema hutunukiwa kwa maofisa wasiokuwa na kamisheni
walio katika utumishi wa JWTZ na wakaguzi, wakaguzi wasaidizi, stesheni sajini,
sajini na koplo wa polisi na magereza.
No comments:
Post a Comment