Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt
Magufuli akiwasalimia maelfu ya Wananchi waliofika katika uwanja wa
Barafu mjini Igunga,Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao.
Mgombea
Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli akisisitiza mbele ya maelfu ya
Wakazi wa mji wa Igunga jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara kuwa
Serikali ya awamu ya tano itajenga viwanda mbalimbali vikiwamo viwanda
vya nguo ikiwa ni mkakati wa kuinua zao la pamba ambalo linalimwa kwa
wingi mikoa ya kanda ziwa,amesema kuwa Serikali yake imedhamiria kuleta
mabadiliko bora na si bora mabadiliko na kuongeza kazi kubwa
atakayofanya ni kusimamia vema rasilimali za nchi kwa maslahi ya
Watanzania wote.
Dkt
Magufuli kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara akiwa katika
wilaya ya Maswa na kisha jimbo la Kishapu na Igunga, Dk.Magufuli amesema
kuwa anatambua umuhimu wa kuwa na viwanda nchini na hivyo serikali yake
itasimamia ujenzi wa viwanda kwa lengo la kuimarisha uchumi na wakati
huo huo kusaidia wakulima na wafugaji kunufaika na shughuli wanaofanya
nchini.
Dk
Magufuli akizungumza na wananchi wakati akijinadi mjini Malampaka,
Maswa, ambapo alisema akishinda urais ataanzisha viwanda vingi ili
kuongeza thamani ya mazao nchini.
Dk
Magufuli akihutubia wananchi katika Mji wa Maganzo mkoani Shinyanga,
ambapo aliomba kumpigia kura ali ashinde awasaidie kuboresha sekta ya
uchimbaji madini kwa serikali kuwakopesha wachimbaji wadogo wadogo kwa
kuwapatia mitaji na vifaa.
Wakazi
wa Maganzo wakiwa wamefunga barabara wakitaka kumsikiliza Mgombea Urais
wa CCM,Dkt John pombe Magufuli alipokuwa akipita kuelekea Igunga mkoani
Tabora kwenye mkutano wa hadhara
Mgombea
urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli (katikati)
akishangiliwa na wananchi wenye ujumbe wa kumuunga mkono huku akiwa na
mfano wa msumeno wa kuwakatia wezi na mafisadi akishinda urais wakati
wa mkutano wa kampeni mjini Igunga , Tabora jioni ya leo.
Wananchi wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa mkutano wa kampeni za CCM mjini Maswa
Wakazi wa Kishapu wakishangilia jambo mara baada ya Mgombea Urais wa CCM kuwahutubia wananchi hao mapema leo mchaa.
Wananchi
wa Kishapu wakimsikiliza kwa makini wakati Dk Magufuli alipokuwa
akijinadi na kuelezea jinsi serikali ya CCM itakavyoboresha sekta
mbalimbali nchini
Sehemu ya umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni za CCM wilayani Igunga leo
Msafara
wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ukiwasili kwenye uwanja wa Barafu
mjini Igunga jioni ya leo,kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
mkoani Tabora.
No comments:
Post a Comment