Na Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini aliyekuwa mkoani Shinyanga.
Mgodi
wa dhahabu wa Buzwagi kupitia idara yake ya mahusiano ya
Jamii imezindua mashindano ya mpira wa miguu na ule wa pete, kwa timu
kutoka kata ya Mwendakulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Ligi
hiyo ambayo imepewa jina la Mahusiano Cup, ikiwa na ujumbe wa
Kuhamasisha masuala ya Usalama, Mahusiano na Maendeleo baina ya wenyeji
na mgodi wa Buzwagi itahusisha timu tisa za mpira wa miguu na timu nane
za mpira wa pete, ambapo kupitia ligi hiyo itaundwa timu moja ya kata
ambayo itakuwa ikishiriki ligi za wilaya.
Akizindua
ligi hiyo Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Amos John
amesema, kupitia mashindano hayo ambayo yamelenga kujenga mahusiano
baina ya Mgodi na wenyeji kwa kuimarisha usalama na kuhamasisha shughuli
za maendeleo miongoni mwa jamii.
Aidha
kaimu meneja huyo amewaasa vijana hao kuonyesha uwezo mkubwa wakati
wote wa mashindano kwani kupitia michezo hiyo baadhi ya vijana
watakaofanya vizuri watachaguliwa kuunda timu ya kata hiyo ambayo
itakuwa ikishiriki michezo mbalimbali kwa ngazi ya wilaya.
Awali
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Bwana Julius
Masubo Kambarage ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada
ambazo imekuwa ikifanya katika kuhamasisha na kuchangia shughuli
mbalimbali za maendeleo ikiwemo michezo.
“Sisi
kwetu kupata mashindano kama haya ni fursa ya pekee sana katika
kuhakikisha shughuli za michezo katika halmashauri yetu zinatekelezwa.
Tutakacho kifanya kwa sasa ni kuhamasisha hizi timu zisajiliwe ili
baadae ziweze kushiriki mashindano makubwa kwa sababu miongoni mwa hawa
vijana wapo wenye vipaji vikubwa ila ni fursa tu hawajapata” Alisema
Kambarage.
Kwa
Upande wake Mratibu wa Mashindano hayo ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo
cha Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Buzwagi Bwana Bahati Mwambene amezitaja
timu zinazoshiriki mashindano hayo kuwa ni Tembo,Star Boys,Shehena, zote
kutoka mtaa wa Chapulwa. Timu nyingine amezitaja kuwa ni Majimaji,
Unity, Budushi, za mtaa wa Mwendakulima, na nyingine ni Israel, Busalala
na Miembeni zote hizi ni kutoka mitaa ya Busalala na Mwime.
Aidha
Bwana Mwambene amesema kabla ya Kuanza kwa mashindano hayo timu zote
zimekabidhiwa vifaa mbalimbali vya michezo kama vile seti za jezi kwa
timu zote pamoja na mipira, ambavyo amesema pamoja na zawadi za washindi
vimegharimu zaidi ya shilingi za kitanzania milioni ishirini na mbili
na laki sita.
Ligi
hiyo ambayo inafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mwendakulima
imeanza tarehe 23 mwezi wa nane na inatarajiwa kumalizika tarehe 05
mwezi wa tisa ambapo mshindi wa kwanza kwa kila mchezo atajinyakulia
kikombe pamoja na pesa taslimu laki tatu, huku mshindi wa pili akiondoka
na laki mbili na nusu na mshindi wa tatu akiondoka na shilingi laki
mbili.
|
No comments:
Post a Comment