Matukio: Wafanyakazi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii Tanzania Wajengewa Uwezo wa Utendaji Kazi - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 26 August 2015

Matukio: Wafanyakazi wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii Tanzania Wajengewa Uwezo wa Utendaji Kazi

 Mwenyekiti wa Jumuiya  ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA),Eliud Sanga  ( kati kati) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa(LAPF), akibadilishana mawanzo na  Katibu mkuu wa  TSSA, Meshack Bandawe, ( kulia) ambaye pia ni Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa ,  Augosti 24, mwaka huu mjini Morogoro  baada ya mwenyekiti huyo kufungua mafunzo kwa wafanyakazi wa mbalimbali wa mifuko yote ya hifadhi ya jamii chini inayounda  Jumuiya hiyo ( kushoto) ni Ofisa Matekelezo wa Mfuko wa PSPF Makao makuu Dar es Salaam.

Na John Nditi, Morogoro
JUMUIYA ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) umewataka vijana wanaoajiriwa katika mifuko inayounda jumuiya hiyo kuingiza mawazo mapya ya ubunifu  katika  kubuni mbinu mbadala za vivutio ili kukubalika katika soko  katika maeneo ya vijijini ambako huduma hizo  hazijawafikia watu wengi.

 Hayo yalisemwa na Mwenyekiti  wa TSSA,  Eliud Sanga , Augosti 24,mwaka huu , wakati alipofungua mafunzo ya siku tano kwa wafanyakazi mbalimbali wa kutoka mifuko yote ya hifadhi ya jamii chini inayounda  Jumuiya hiyo . 

 Alisema kuwa,  soko bado ni kubwa la kutatafuta wanachama walio nje ya ajira isiyorasmi kuwaingiza katika mifuko hiyo hivyo ni vyema  wakaanza kuelekeza nguvu zao katika kutafuta wanachama  maeneo ya vijijini ambako kuna idadi kubwa ya wananchi wanaohitaji huduma zao.

  Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa hifadhi ya wafanyakazi wa Serikali za Mitaa(LAPF), alisema si jambo jema kuendelea   kulumbuna na  kugombania wanachama katika maeneo ya mijini kwani soko bado ni kubwa maeneo ya vijijini ambapo kuna ajira binasfi na isiyo rasmi. 

 Alisema  endapo vijana wasomo wanaoajiriwa katika mifuko hiyo wanaingiza mawazo mapya na ubunifu wao , kila mfuko utakuwa na hazina kubwa ya wanachama kutokana na  kuwafikia wananchi wanaoishi katika maeneo ya vijijini ambao ni wakulima na wafugaji wenye uwezo wa kuchangia mifuko hiyo.

Mwenyekiti huyo wa TSSA , alisema  kutokana na mifuko hiyo kujikita katika maeneo ya mjini imekuwa ikitoa huduma hiyo kwa asilimia nne pekee  na endapo itaongeza juhudi za kuwafikia watu wa maeneo ya vijijini inaweza kufikia zaidi ya asilimia 96.

Alisema , kuna kundi kubwa la wakulima,wafugaji na waendesha bodaboda ambao mifuko hiyo inapaswa  kwenda kuhamasisha  kujiunga na kuchangia huduma hizo za  hifadhi ya jamii  na pia kuangalia namna ya kutangaza mafao hayo. 

Naye  Katibu Mkuu wa TSSA, Meshack Bandawe, alisema  malengo ya kuanzisha Jumuiya hiyo ni kufanya kazi kwa pamoja na kwa lengo moja ili kuhakikisha sekta ya hifadhi ya jamii inaimarishwa ili kuingiza Watanzania katika mifuko hiyo na waweze kunufaika nayo.
Mafunzo hayo ya siku tano  yanawashirikisha wafanyakazi  kutoka mifuko ya NSSF, PPF, LAPF, GEPF,NHIF na ZSSF na yamelenga kuwagengea uwezo wa ufahamu mkubwa juu ya madhumuni, malengo , umuhimu na misingi ya sekta ya hifadhi ya jamii ili kuboresha utendaji wao wa kazi katika sekta ya hifadhi ya jamii ili kuwafanya watanzania wengi wafaidike.

Bandawe ambaye pia ni Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa,alisema kuwa kupitia Jumuiya hiyo sasa wataanza kuwaelimisha wananchi wote walioko rasmi katika soko ajira na wale wasio rasmi waweze kukingwa na mifuko ya hifadhi ya jamii .

Alisema kuwa wanaangalia namna ya kuiboresha mifuko hiyo kwa kupata uzoefu jinsi mifuko hiyo inavyofanya kazi katika nchi za Afrika mashariki  ambayo imekuwa ikisaidia sana wananchi hasa wanaoishi katika maeneo ya vijijini.

Katibu mkuu huyo  alisema,  kupitia mafunzo hayo wanaangalia namna ya kupata wanachama ambao ni Watanzania wanaoishi nje ya nchi kuweza  kuchangia kwenye mifuko hiyo wakiwa huko huko na wale wanaoishi maeneo ya vijijini.

No comments:

Post a Comment