Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto) akisalimiana na Kaimu Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), Mary Mtukula
alipowasili katika eneo la Mtambo wa Ruvu juu Darajani Wilayani Bagamoyo
Mkoa wa Pwani Agosti 25, 2015 wakati wa ziara ya siku tatu ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa miradi ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam
ambapo miradi hiyo inasimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
(DAWASA).
Ujenzi uifadhi wa pampu ukiendelea.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla akikagua moja ya transfoma ya umeme
kwaajili ya kuongeza uwezo wa utendaji kazi wa mashine mpya zitakazo
fungwa,Waziri Amos Makalla anafanya ziara siku tatu ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa miradi ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam
ambapo miradi hiyo inasimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
(DAWASA).
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akipata maelezo kutoka kwa Meneja Usimamizi Uendeshaji na Mazingira DAWASA, Modesta Mushi kuhusiana na upanuzi wa mtambo wa kuongeza uzalishaji kutoka mita za ujazo 82,000 hadi 196,000 kwa siku.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla akiwa ameongozana na wakandarasi wa miradi
na maofisa kutoka Wizara ya maji. wakikagua ujazo wa maji ruvu Darajani.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla pamoja na wakandarasi wa miradi na maofisa
kutoka Wizara ya maji. wakikagua wakiangalia kina cha maji kilipofikia.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla (wa pili kushoto) akiwa ameongozana na
Meneja mradi wa Kampuni ya WABAG kutoka India. Pintu Dutta (watatu
kulia) Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
(DAWASA), Mary Mtukula, Injinia Masudi Omari, Meneja Usimamizi
Uendeshaji na Mazingira DAWASA, Modesta Mushi wakikagua maendeleo ya
mradi wa kituo cha kusafisha maji cha ruvu juu .
Wakiwa ndani ya Mtambo wa zamani wa kusukuma maji.
Ujenzi wa nyumba za wafakazi ukiendelea.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto), akiwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), Mary Mtukula wakitafakali
jambo kabla ya kuanza mazungumzo na wakandarasi wanaojenga mradi huo.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla meza kuu mbele akifanya mazungumzo na
maofisa wa Kampuni ya WABAG mara baada ya kufika katika eneo la upanuzi
wa mtambo wakuongeza uzalishaji wa maji ulipo Mlandizi pamoja na
kujionea ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na matanki ya machujio ya maji.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa matanki ya maji.
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia) akizungumza na waandishi wa habari
mara baada kukagua upanuzi wa mtambo wakuongeza uzalishaji wa maji ulipo
Mlandizi pamoja na kujionea ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na matanki
ya machujio ya maji.
Mafundi wa Kampuni ya Megha Engenearin Infastructure wakiendelea na ulazaji wa mabomba mapya ya maji eneo la Tumbi Kibaha.
Kutoka
kulia ni Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Megha Engenearin Infastructure
Limited Mural Mohan, akimweleza maendeleo ya mradi huo Naibu Waziri wa
Maji, Amos Makalla wakati wa ziara ya siku tatu ya kukagua maendeleo ya
ujenzi wa miradi ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo miradi hiyo
inasimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA). Picha zote
na Alex John
No comments:
Post a Comment