Maelefu ya wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA, wakiwa wamefurika katika Hoteli ya Kiss, iliyoko Kiborloni, mjini Moshi mara baada ya Mgombea wa Urais wa UKAWA, kupitia Chadema, Waziri Mkuu wa Zamani , Edward Lowassa, Kuwasili hotelini hapo kwa ajili ya mapumziko kabla ya kuelekea Usangi kuhudhuria Mazishi ya Peter Kisumo. |
Msafara wa Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa ukielekea Kiss Hotel, mara baada ya kuwasili mjini Moshi kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). |
Mbunge wa Jimbo la Rombo (Chadema), akikimbia kwa miguu wakati Msafara wa Lowassa, ukielekea Kiss Hotel. |
Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa akiwasili Kiss Hotel, kabla ya kuanza safari ya kuelekea Usangi. |
Mheshimiwa Lowassa akipata maelezo mafupi kutoka kwa Katibu wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Basil Lema. |
Safari ya Lowassa kuelekea Usangi kutoka katika Hoteli ya Kiss ikaanza |
Msafara wa Lowassa ukielekea Usangi
|
Ghafla msafara wa Lowassa na viongozi wengine wa UKAWA, pamoja na Pikipiki zaidi ya 100, ukazuiwa na Jeshi la Polisi katika Kijiji cha Maroro, kilomita moja kutoka Mwanga mjini kelelekea Ugweno. |
Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Mwanga (OC-CID), akiwa na askari wa Jeshi la Polisi |
Askari wa FFU wakiwa wamezuia msafara wa Lowassa. kwenye picha linaonekana Landrover la Polisi likiwa limefunga njia. |
Wananchi waliamua kulala Barabarani, wengine wakiwa wamekaa mbele ya gari la Jeshi la Polisi huku viongozi wakihaha kupata Ufumbuzi. |
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia (katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Mwanga (jina halijafahamika) pamoja na baadhi ya viongozi wa Chadema. |
Mwenyekiti wa TLP, Dkt. Augustino Mrema, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia pamoja na Henry Kilewo wakishauriana baada ya msafara wa Lowassa kuzuiliwa. |
No comments:
Post a Comment