Matukio /Siasa :Dk. John Pombe Magufuli wa CCM, Mhe Edward Lowassa wa CHADEMA na Lyimo wa TLP waliporudisha fomu zao tume ya uchaguzi - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 22 August 2015

Matukio /Siasa :Dk. John Pombe Magufuli wa CCM, Mhe Edward Lowassa wa CHADEMA na Lyimo wa TLP waliporudisha fomu zao tume ya uchaguzi

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva akijadili Jambo na Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Hamid Mahmoud Hamid wakati wa urudishaji wa fomu za kugombea nafasi ya Urais Kuelekea Katika Uchaguzi Mkuu wa Octoba 25, 2015.

Mgombea Urais  Kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa Uchaguzi Damian Lubuva wakati wa kurejesha Fomu za kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mapema leo kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jijini Dar es Salaam.

Mgombea Kupitia Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli akipokea nyaraka mbalimbali ikiwemo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,Maelekezo kwa wagombea wa vyama vya siasa, Maadili ya Uchaguzi toleo la mwka 2015 na sheria na kanuni za gharama za uchaguzi kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa Uchaguzi Damian Lubuva, mapema leo kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jijini Dar es Salaam.

Mgombea Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akipokea nyaraka mbalimbali toka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa Uchaguzi Damian Lubuva, mapema leo kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jijini Dar es Salaam.

Mgombea Urais Kupitia chama cha TLP Bw. Macmillan Elifatio Lyimo (Kushoto) akipokea nyaraka mbalimbali toka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa Uchaguzi Damian Lubuva, mapema leo kwenye ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment