Utalii na Maisha : TREK4MANDELA Watembelea Shule ya Sekondari Darajani Iliyopo Marangu - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


17 Jul 2015

Utalii na Maisha : TREK4MANDELA Watembelea Shule ya Sekondari Darajani Iliyopo Marangu


Timu ya watu 39 Wakiwemo wakurugenzi wa Taasisi na wakurugenzi kampuni mbalimbali za nchini Afrika Kusini walipotembelea shule ya sekondari ya Mazoezi Darajani iliyopo Marangu wilaya ya Moshi.
Baadhi ya wanafunzi katika shule ya sekondari ya Mazoezi Darajani iliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro wakiwa darasani.
Wananfunzi katika shule ya sekondari Darajani wakiwa katika mkusanyiko tayari kupokea wageni waliotembelea shule hiyo.
Mhifadhi katika Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro,KINAPA ,Charles Ngendo akiwatambulisha wageni kutoka Afrika Kusini mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Darajani.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa,TANZANIA,(TANAPA) Allan Kijazi akiwa na ugeni kutoka nchini Afrika kusini walipotembelea shule ya sekondari ya Darajani iliyopo Marangu.
Mkuu wa shule ya sekondari ya Darajani iliyopo Marangu,Mary Mlay akisoma taarifa ya shue hiyo mbele ya wageni waliotembelea shule hiyo.
Katibu Tawala wilaya ya Moshi,Remida Ibrahim akizungumza wakati ugeni wa timu ya watu 39 ulipotembelea shule ya sekondari Darajani kwa lengo la kusaidia kununua taulo maalumu za wasichana waliopo mashuleni pindi wawapo katika siku zao za Hedhi.


Mwanzilishi wa taasisi ya Imbumba Foundation ,Richard Mabaso ambaye taasisi yake inaratibu zoezi la upandaji Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia kununua taulo maalumu kwa wasichana walio mashuleni.
Mwakilishi wa jiji la Ekurhuleni nchii Afrika Kusini,Lebo Modibe akikabidhi vipeperushi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa,Tanzania (TANAPA)Allan Kijazi ambavyo viligawiwa kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa ,Tanzania(TANAPA) Allan Kijazi akimshukuru Mwanzilishi wa taasisi ya Imbumba Foundation na Nelson Mandela Foundation kwa kuchangia msaada wa ununuzi wa taulo maalumu kwa wasichana waliopo mashuleni pindi wawapo katika siku zao za Hedhi.
Katibu tawala wilaya ya Moshi ,Remida Ibrahim akikabidhi vipeperushi kwa walimu wa shule hiyo.


Mcheza filamu maarufu wa nchini Afrika Kusini,Jacky Davnarain maarufu kama Rajesh wa tamthiliya ya Isidingo pia ni miongoni mwa wageni hao wanaopanda Mlima Kilimanjaro.


Na Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad