MABALOZI
wa Usalama Barabarani nchini Tanzania (Road Safety Ambasadors-RSA)
wamekabidhi misaada kwenye Ofisi ya Kitengo cha Mawasiliano cha Kikosi
cha Usalama Barabarani cha Jeshi la Polisi nchini (Traffic Control
Center-TCC).
Vifaa
hivyo ambavyo ni vitendea kazi katika kituo cha taarifa cha Kitengo cha
Mawasiliano cha Kikosi cha Usalama Barabarani cha Jeshi la Polisi
nchini, vimekabidhiwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa RSA,
John Seka ikiwa ni michango ya mabalozi hao.
Akizungumza
katika hafla hiyo ya kukabidhi, Seka alisema lengo la msaada huo ni wa
Mabalozi wa Usalama Barabarani ni kutaka kuboresha mawasiliano ya Jeshi
la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani.
Alivitaja
vifaa vilivyokabidhiwa kuwa ni pamoja na Radio mbili za mawasiliano za
kidijitali, Simu ya mawasiliano aina ya Tablet iliyounganishwa na
makundi ya RSA ya Facebook, Whatsapp na Telegram, Mtungi wa Maji ya
Kunywa, Viti vya kukalia, Feni na Zulia la Ofisi ya TCC.
Aidha
Seka alitaja msaada mwingine ni Birika la kuchemsha maji ya chai, Mfumo
wa kutunza betri kwa ajili ya Tablet (Power Bank) na Gharama za Upakaji
wa Rangi wa ofisi ya TCC ikiwa vyote vinalenga kuhakikisha ofisi ya TCC
inafanya kazi kwa ufanisi na bila vikwazo ili kurahisisha mawasiliano
kati ya RSA na TCC.
"RSA
ni mkusanyiko wa watanzania wanaotumia mitandao ya kijamii yaani Social
Media katika mawasiliano. Hawa ni Watanzania wanaoamini kuwa mitandao ya
kijamii ya Facebook, Whatsap na Telegram inaweza kutumiwa kuleta
mabadiliko katika jamii.
Huu ni
mtazamo chanya ulio na lengo la kuhakikisha kuwa tunabadili mtazamo wa
kuwa mitandao ya kijamii inatumika vibaya," alisema Seka akifafanua juu
ya RSA.
Aliongeza
kuwa RSA ilitambulishwa rasmi tarehe 17 October 2013 na kuzinduliwa
rasmi tarehe 28 Desemba 2014 katika ukumbi wa bwalo la Maofisa wa Polisi
Oysterbay na hadi sasa ina zaidi ya wananchama 5000 walioko Facebook,
wanachama 500 katika group la Whatsapp la kitaifa na yale ya mikoani na
pia wanachama 400 wako Telegram.
"...Kinachofanywa
na RSA ni kuhakikisha kuwa tunawapa watanzania ujasiri wa kuripoti
matukio ya uvunjifu wa sheria na kanuni zinazoratibu usalama wa
watanzania wakiwa barabarani. Kwa kutumia simu zao wanaRSA hupiga picha
za matukio ya uvunjifu wa sheria za barabarani na kuzituma kwenye haya
magroup niliyoyaelezea hapo juu." Alisema Mwenyekiti huyo wa RSA katika
taarifa yake.
mabalozi
wa RSA wakikabidhi vifaa hivyo kwa maofisa wa Kitengo cha Taarifa cha
Kikosi cha Usalama Barabarani cha Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment