Mkuu
wa Vodacom Tanzania Kanda ya kati, Mruta Hamisi ( aliyesimama kulia)
akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula
iliyofanyika katika mikoa mitatu Nchini na kumalizikia katika mikoa ya
kanda ya kati, mjini Dodoma jana.Waliokaa ni Naibu Waziri wa Afya na
Ustawi wa jamii, Dk Stephen Kebwe (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa
CCBRT, Erwin Telemans.Kampeni hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Hospitali ya
CCBRT na Vodacom Foundation ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa Umma na
kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe
maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000
kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe (aliyesimama)
akizunguza wakati wa kuhitimisha kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula
katika mikoa ya kanda ya kati, mjini Dodoma jana. Waliokaa kutoka
kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans, Mkuu wa
Vodacom Tanzania Kanda ya kati, Mruta Hamisi na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la UNFPA, Rutasha Dadi. Kampeni hiyo ilikuwa
ikiendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ilifanyika
katika mikoa mitatu ikiwa na dhumuni la kutoa elimu kwa Umma na
kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe
maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000
kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
Wakazi
wa manispaa ya Dodoma wakihudhuria kwa wingi kwenye hitimisho la
kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula. Ambapo Naibu Waziri wa Afya
Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe alihitimisha kampeni hizo katika
viwanja vya Mashujaa mjini Dodoma jana. Kampeni hiyo iliyokuwa
ikiendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ilifanyika
katika mikoa mitatu ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa Umma na
kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe
maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000
kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
Wananchi
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe
wakati kuhitimisha kampeni ya maradhi ya Fistula iliyofanyika kwa
kuzunguka katika mikoa mitatu nchini na kuhitimishwa katika mikoa ya
kanda ya kati, mjini Dodoma jana. Kampeni hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na
Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ilikuwa na lengo la kutoa elimu
kwa Umma na kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili
wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya
wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
Wasanii
wa kundi la Mjomba band, wakiigiza kwa kufukuzwa kwa mwanamke
aliyekuwa na maradhi ya Fistula, na mumewe ikiwa ni ishara ya
kunyanyapaliwa kwa wenye maradhi hayo katika jamii. Onyesho hilo
lilifanyika mjini Dodoma jana wakati wa hitimisho ya kampeni dhidi ya
maradhi ya Fistula iliyofanyika katika mikoa mitatu Nchini na
kumalizikia katika mikoa ya kanda ya kati mjini Dodoma. Kampeni hiyo
ilikuwa ikiendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ilikuwa
na lengo la kutoa elimu kwa Umma na kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu
wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika.
Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi
hayo wanapojifungua.
No comments:
Post a Comment