Mkotya
ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari na kijana msomi mwenye Shahada
ya Siasa na Uongozi, alitangaza nia hiyo mbele ya waandishi wa habari,
katika ukumbi wa Dodoma Hotel.
Mkotya ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi ni miongoni mwa waandishi wa habari za Bunge, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuwatetea wananchi wa Chemba kupitia taaluma yake.
Mkotya ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi ni miongoni mwa waandishi wa habari za Bunge, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuwatetea wananchi wa Chemba kupitia taaluma yake.
Akizungumza
katika mkutano huo, Mkotya ambaye ni mzaliwa wa Kijiji cha Mirijo Chini
wilayani Chemba, alisema changamoto za jimbo hilo ndizo zilizomsukuma
kuwania nafasi hiyo.
Katika
mkutano huo, Mkotya alisema kwa muda mrefu ametumia taaluma yake kupiga
kelele kuibua matatizo na kero za wananchi wa Chemba na baadhi kupatiwa
ufumbuzi, hivyo umefika muda kuomba ridhaa yao ili aweze kuwatumikia
kimamlaka zaidi.
Uzoefu
wake katika masuala ya Bunge kama mwandishi wa habari za Bunge, pia
utakuwa chachu na msaada mkubwa kwake katika kutimiza dhana ya
uwakilishi ndani ya Bunge.
Ndugu
zangu sijakurupuka katika kufikia uamuzi huu, nimekaa, nimetafakari na
kujipima mwenyewe na kubaini kwamba ninatosha. Uwezo wa kutekeleza
majukumu ya kibunge ninao, nia ya kuwatumikia wananchi wa Chemba ninayo
na sababu za kugombea ninazo.
Endapo
nitafanikiwa kupata ridhaa ya chama changu, baada ya kupitia mchakato
wa kura za maoni na baadaye kushinda uchaguzi wa nje, nitajitahidi
kutimiza wajibu wangu ipasavyo.
Natambua
kero nyingi zinazowazonga wananchi wa Chemba kama vile shida ya maji,
uduni wa huduma za afya, miundombinu mibovu ya barabara, anguko la
elimu, ukosefu wa masoko ya mazao na migogoro ya wakulima na wafugaji.
Katika
kuhakikisha tunaondoa changamoto hizo, kipaumbele changu cha kwanza ni
maji. Naamini tatizo la maji likimalizika , itawafanya wananchi kufanya
shughuli nyingine za maendeleo, kwani hivi sasa uchumi wao mwingi
unaishia katika maji.
Pili,
nitasimamia ipasavyo fedha za Mfuko wa Jimbo ili ziweze kufanya kazi
iliyokusudiwa na Serikali, katika kuharakisha maendeleo na kuboresha
huduma kwa wananchi, kama ilivyoainishwa katika Sheria namba 16 ya mwaka
2009 ya Mfuko wa Jimbo (CDCF).
Tatu,
mbali na kufanya jitihada nyingine za kupata fedha kwa ajili kusukuma
maendeleo yetu, nitatumia uwezo wangu wote kuisimamia halmashauri yangu
ya wilaya, iweze kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya
kuwawezesha vijana na wanawake kujiunua kiuchumi.
Nne,
nakusudia kurejesha imani ya wananchi wa Chemba kwa Chama Cha
Mapinduzi, ambayo imetikiswa katika kipindi hiki cha miaka mitano. Hii
ni kutokana na aina ya uongozi wa kisiasa wa sasa uliotawaliwa na ubabe
zaidi badala ya mbinu shirikishi.
Chama
Cha Mapinduzi ni chama kilichojengwa katika misingi ya usawa na umoja,
hivyo katika ushindani wa kisiasa wa sasa ni vigumu chama kushinda, kwa
kuendeleaa kukumbatia viongozi wasiokuwa waadilifu na wanyenyekevu kwa
wananchi.Chemba
kama wilaya inahitaji mbunge mwajibikaji, mchapakazi, mtu jasiri,
mwenye uadilifu usiokuwa na shaka na anayejua matatizo ya watu wa
Chemba.
Sina
shaka na uadilifu wangu, uwezo wangu na wala uzalendo wangu si wa
kuokoteza. Maendeleo ni mchakato (process), binafsi naamini katika U3
ili kufikia maendeleo. Ukweli, Uwazi na Uwajibikaji.
Viongozi
pamoja na wananchi wote kwa ujumla wetu tukiishi katika U3, naamini
maendeleo yatapatikana. Kupitia waraka huu natangaza rasmi nia ya
kugombea ubunge Jimbo la Chemba katika uchaguzi mkuu wa 2015.
No comments:
Post a Comment