Matukio : Wizara ya Nishati na Madini Yazindua Huduma za Leseni kwa Njia ya Mtandao - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Tuesday, 9 June 2015

Matukio : Wizara ya Nishati na Madini Yazindua Huduma za Leseni kwa Njia ya Mtandao


Kikundi cha Ngoma za Asili cha Simba kutoka Dodoma (kushoto) kikitumbuiza mbele ya Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia katikati, aliyevaa koti la kahawia) kabla ya uzinduzi wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao uliofanyika mjini Dodoma.
Kamishna Msaidizi wa Madini- Kitengo cha Leseni, Mhandisi John Nayopa (Kulia) akielezea mfumo wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao unavyofanya kazi kabla ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka kushoto, aliyekaa meza kuu).
Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja (Kulia) akielezea mafanikio katika uboreshaji wa huduma za utoaji leseni kwenye uzinduzi huo.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akisoma hotuba ya uzinduzi wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao. Wa pili kutoka kulia ni Kamishna wa Madini Nchini, Mhandisi Paul Masanja na wa kwanza kushoto mbele ni Kamishna Msaidizi wa Madini- Kitengo cha Leseni, Mhandisi John Nayopa.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa nne kutoka kulia, waliokaa mbele); Kamishna wa Madini Nchini Mhandisi Paul Masanja ( wa tano kutoka kulia, waliokaa mbele) na Kamishna Msaidizi wa Madini- Kitengo cha Leseni, Mhandisi John Nayopa ( wa pili kutoka kushoto, waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini waliohudhuria uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment