Matukio : Taswira ya Ziara ya Rais Jakaya Kikwete nchini Finland - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 3 June 2015

Matukio : Taswira ya Ziara ya Rais Jakaya Kikwete nchini Finland

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Finland, Balozi Dorah Msechu katika uwanja wa ndege wa Helsinki, wakati alipowasili tayari kwa ziara ya siku tatu nchini humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi maafisa wa Serikali ya Finland katika uwanja wa ndege wa Helsinki, wakati alipowasili tayari kwa ziara ya siku tatu nchini humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea maabara ya majaribio ya kampuni ya kutengeza lifti ya KONE jijini Helsinki, Finland.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya jezi ya timu ya taifa ya Finland ya basketball.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa zawadi ya mchoro wa Tingatinga kwa viongozi wa kampuni ya KONE.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea bandari ya Helsinki
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata mapokezi Rasmi kutoka kwa mwenyeji wake, Rais wa Finland Mhe. Sauli Niinisto.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha mwenyeji wake, Rais wa Finland Mhe. Sauli Niinisto kwa ujumbe alioambatana nao Ikulu ya Finland.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake, Rais wa Finland Mhe. Sauli Niinisto.
PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment