Mfuko wa Jamii : Mkutano wa 5 wa Wadau wa NSSF Unaendelea , Jijini Arusha - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 3 June 2015

demo-image

Mfuko wa Jamii : Mkutano wa 5 wa Wadau wa NSSF Unaendelea , Jijini Arusha


MMGL0108
Mgeni rasmi kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa tano wa Wadau wa NSSF, Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mh. Joshua Nassary wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha leo. Kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudencia Kabaka na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ndg. Aboubakar Rajab pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau.
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda na ujumbe wake wakiangalia burudani ya ngoma kabla ya kuingia ukumbini.
MMGL0188
Sehemu wa Wadau wa Mkutano Mkuu wa tano wa NSSF wakishiriki kwa pamoja kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mkutano huo.MMGL0603
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akitoa hotuba yake ya Ufunguzi wa Mkutano wa tano wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.Mh. Pinda awewasihi wasomi nchini pamoja na watanzania  kuacha fikra ya kusubiri kuajiriwa mara wanapomaliza vyuo badala yake wajiajiri wenyewe ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha.
MMGL0325
Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudencia Kabaka akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda ili aweze kuufungua Mkutano wa tano wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.MMGL0854
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ndg. Aboubakar Rajab akitoa shukrani kwa Mgeni Rasmi, Wajumbe na Wadau walioshiriki kwenye Mkutano wa huo, ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
MMGL0292
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akizungumza mapema leo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa tano wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo, kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha. Dkt. Dau amesema, NSSF kwa sasa imeanza kutoa mikopo kwa wajasiriamali na imeshatoa mikopo kwa wanachama wake yenye thamani ya Sh. bilioni 55.6.
MMGL0296
Dkt. Dau akiendelea kuzungumza.
MMGL0302
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi wakifatilia Mkutano huo.
MMGL0524
Mmiliki wa Hoteli ya Peacock, Mzee Joseph Mfugale akitoa ushuhuda wake wa ujasiriamali katika Mkutano wa tano wa Wadau wa NSSF, ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
MMGL0558
Mmiliki wa Kampuni ya SSTL Group, Bw. Almas Maige akitoa ushuhuda wake wa ujasiriamali katika Mkutano wa tano wa Wadau wa NSSF, ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
MMGL0570
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda na Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudencia Kabaka wakisikiliza kwa umakini ushuhuda wa ujasiriamali uliokuwa ukitolewa na Mzee Joseph Mfugale pamoja na Bw. Almas Maige, wakati wa Mkutano wa tano wa Wadau wa NSSF, ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
MMGL0348
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akifatilia hotuba ya Mgeni Rasmi, Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda.
MMGL0354
Wadau wakifatilia Mkutano.
Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudencia Kabaka.
MMGL0401
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Makongoro Mahanga.
MMGL0434
MMGL0497
Mkutano ukiendelea.
MMGL0516
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF, Bw. Aboubakar Rajab.
MMGL0575
Dkt. Dau akisikiliza Ushuhuda wa ujasiriamali uliokuwa ukitolewa na Mzee Joseph Mfugale pamoja na Bw. Almas Maige, wakati wa Mkutano wa tano wa Wadau wa NSSF, ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
MMGL0581
Wadau wa Mkutano wa tano wa NSSF wakifatilia kwa umakini ushuhuda wa ujasiriamali uliokuwa ukitolewa na Mzee Joseph Mfugale pamoja na Bw. Almas Maige, leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.

MMGL0677
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya Muajiri bora Sekta ya Utali, kwa Afisa Mwajiri wa Hifadhi ya Grumeti, Bw. Som Kakiva.
MMGL0683

MMGL0687
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akikabidhi tuzo ya Ubora wa Sekta ya Afya, Meneja Muajiri wa Hospitali ya Agha Khan, Bi. Mary Mlay.
MMGL0703

MMGL0730

MMGL0741

Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi mfano wa kadi ya Hifadhi ya wastaafu (Hifadhi Smart Card), Bi. Kessi-Sia Mbatia (kushoto), itakayomuwezesha Mstaafu kujipatia Fedha zake za pensheni kwa haraka, wakati wa Uzinduzi wa huduma hiyo mpya itakayokuwa ikitolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Wengine pichani kutoka kulia ni Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudencia Kabaka, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ndg. Aboubakar Rajab pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau.
MMGL0817
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akishuhudia namna Kadi ya Wastaafu inavyofanya kazi kupitia  ATM za Selcom zitakazokuwe maeneo mbali mbali nchini ili kuwawezesha wastaafu kujipatia Fedha zao za pensheni kwa haraka, wakati wa Uzinduzi wa huduma hiyo mpya itakayokuwa ikitolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ndg. Aboubakar Rajab pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau.
MMGL0843
Baadhi wa wawakilishi wa Mifuko ya Hifadhi za jamii.
MMGL0864

MMGL0880
Zawadi kwa Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudencia Kabaka kazi kubwa anayoifanya kusimamia na kuhakikisha Mifuko ya Hifadhi za Jamii inakuwa bora hapa nchini.
MMGL0897
Zawadi kwa Mgeni Rasmi.

MMGL0940


MMGL0974

MMGL0989

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *