Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dk. Donan Mbando akiwa kwenye
picha ya pamoja na madaktari na viongozi wa chuo kikuu cha Afya na
Sayansi shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) mara baada ya kufunga mkutano
mkuu watatu wa sayansi ya afya uliondaliwa na chuo hicho jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Kushoto kwake ni Makamu mkuu wa
MUHAS, Prof. Ephata Kaaya.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dk. Donan Mbando akiwa kwenye
picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa udaktari, madaktari na
viongozi wa chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili
(MUHAS) mara baada ya kufunga mkutano mkuu watatu wa sayansi ya afya
uliondaliwa na chuo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dk. Donan Mbando akiagana na
baadhi ya wanafunzi wa udaktari kutoka chuo kikuu cha Afya na Sayansi
shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) mara baada ya kufunga mkutano mkuu
watatu wa sayansi ya afya uliondaliwa na chuo hicho jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki iliyopita.
Na Mwandishi Wetu,
SERIKALI
imewaomba watafiti wa masuala ya afya hapa nchini kuhakikisha kwamba
wanaibua hoja mpya zitakazosaidia kuleta mabadiliko kwenye sera za
kitaifa zinazohusu sekta hiyo muhimu. Wito huo umetolewa jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa
jamii Dk. Donan Mbando mara tu baada ya kufunga mkutano mkuu watatu wa
sayansi ya afya uliondaliwa na chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi
cha Muhimbili (MUHAS).
“Kwa
sasa taifa linashuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaosumbuliwa
na magonjwa yasiyoyakuwa ya mbukiza kama vile kisukari, shinikizo la
damu na kisukari. Kwa bahati mbaya sana vituo vyetu vingi vya afya
havijaandaliwa vizuri kukabiliana na magonjwa haya kwasababu sera zetu
wakati zinaandaliwa hazikujika zaidi kwenye magonjwa yasiyoyakuwa ya
kuambukiza na ndio maana tunahitaji mabadiliko kwenye hili,’’ alisema Dr. Mbando.
Dr.
Mbando alizataja sababu kubwa zinazochangia ongezeko la magonjwa hayo
kuwa ni pamoja na matumizi ya pombe kupita kiasi, aina ya vyakula
vinavyotumiwa na watanzania hususani wale wanaoishi maeneo ya mijini,
kutokufanya mazoezi pamoja na uvutaji wa sigara. Aidha
aliiongeza kuwa kwa sasa serikali ipo kwenye mpango wa kuandaa mkakati
wanne wa huduma za afya hapa nchini (health care financing strategy)
utakao muwezesha kila mtanzania kuwa na bima ya afya.
“Kwa
sasa ni asilimia 20 tu ya watanzania ndio wanamiliki bima za afya
zinazotolewa na shirika la bima ya afya la taifa na mashirika binafsi na
hivyo kufanya asilimia 80 ya watanzania kuishi bila kuwa na uhakika wa
masuala ya tiba….hili tumelianza tayari,’’ alibainisha.
Kuhusu
mlipuko wa ugonjwa wakipundupindu kwenye mikoa ya kagera na kigoma
uliosababishwa na kuingia kwa wakimbizi kutoka Burundi, Dr. Mbando
alisema kwa sasa serikali kwa kushirikiana na Wananchi, wadau wa
maendeleo na asasi zisizo za kiraia wanapambana kuhakikisha tatizo hilo
linakwisha.
Akizungumza
kwenye mkutano huo Makamu mkuu wa MUHAS, Prof. Ephata Kaaya alisema kwa
sasa taifa linahitaji zaidi tafiti za kiafya hususani kwenye magonjwa
yasiyo ya kuambukiza na ndio sababu mkutano huo ulijikita zaidi kujadili
tatizo hilo.
“Kama
wataalamu wa masuala ya afya tunaona kuna haja kubwa tukiwekeza katika
tafiti zinazolenga kuibua changamoto na suluhisho kwenye magonjwa
haya,’’ alisema. Mkutano huo wa
siku mbili ulihudhuriwa na washiriki zaidi ya 300 wakiwemo madaktari,
viongozi na wanafunzi wa udaktari kutoka MUHAS na vyuo vingine vya afya.
No comments:
Post a Comment