Meneja wa Uwajibikaji na Huduma za Jamii wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy, Andrew Kashangaki(wa katikati) akimkabidhi funguo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega(wa pili kushoto) za jengo la Wauguzi la Zahanati ya Nangurukuru wilayani Kilwa. Wa kanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Peter Malekela, wapili kushoto ni Mbunge wa Kilwa Kusini, Suleman Ally Bungara 'Bwege' na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilwa Mzee Ally Mtopa.[/caption]
Na Mwandishi Wetu, Nangurukuru
KAMPUNI ya Pan African Energy Tanzania Ltd imekabidhi msaada wa jengo lenye nyumba mbili za wahudumu wa afya wa Zahanati ya Nangurukuru ikiwa ni jitihada za kuisaidia Serikali kupunguza vifo vya akinamama na watoto katika eneo la Nangurukulu na vijiji vya jirani. Akikabidhi majengo hayo jana kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Meneja Uwajibikaji kwa Jamii wa Kampuni ya Pan African Energy Tanzania Ltd, Andrew Kashangaki alisema lengo kubwa la misaada wanayotoa ni kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika wilaya ambazo wanafanyia kazi zao. Alisema kuwa madhumuni ya msaada wa ujenzi wa nyumba hizo mbili waliozijenga kwenye Zahanati ya Nangurukuru ni kuimarisha mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka maeneo ambayo wanafanyia shughuli zao. Aidha Kashangaki alisema mradi huo wa ujenzi wa nyumba za waganga umegharimu zaidi ya milioni 458 za fedha za Kitanzania na zimejengwa kisasa ambapo zinauwezo wa kubeba familia nne za watumishi wa Zahanati ya Nangurukuru hali ambayo itasaidia. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Abdulah H. Ulega akipokea nyumba hizo alisema msaada huo utapunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya akinamama wajawazito na watoto eneo hilo ambapo awali vilikuwa vinatokana na huduma za afya kuwa mbali na makazi ya akinamama hao. "...Ni kweli kwamba bado tunatatizo kubwa la vifo vya akinamama na watoto eneo letu na vifo hivi vinachangiwa na tatizo la kukosekana kwa huduma za afya karibu...kama inavyoeleza sera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi. Aliongeza kuwa Wilaya ya Kilwa kwa sasa inajitahidi kuhakikisha suala hilo lakuendelea na ujenzi wa zahanati zaidi unafanya vizuri. "...Na moja ya mafanikio yetu ni ujenzi wa Zahanati ya Nangurukuru na nyingine tano tunazijenga, awali ilikuwa kati ya Vijiji 90 vya Wilaya yetu vilivyokuwa na huduma za afya vilikuwa 43, lakini ndani ya miaka mitatu tumejitahidi kuunga mkono juhudi za wanakijiji walipoanza mchakato wa ujenzi wa zahanati kwenye vijiji vyao," alisema Mkuu wa Wilaya. Kwa upande wao baadhi ya wakazi waliohojiwa katika hafla hiyo ya makabidhiano walisema ujenzi wa nyumba ya watumishi wa zahanati ya Nangurukuru utawasaidia sana kihuduma za afya eneo hilo kwani awali wananchi walikuwa wakilala barabarani wakati mwingine usiku wakisafiri kutafuta huduma za afya. Mwenyekiti wa Kitongoji cha Dodomezi, Mwanahawa Hamis alisema uzinduzi wa jengo la zahanati hiyo utawasaidia hasa akinamama ambao walikuwa wanapoteza maisha njiani kutokana na kutembea umbali kufuatilia huduma za afya. Naye Mwanawetu Mshamu Mkazi wa Kitongoji cha Dodomezi, mbali na kukabidhiwa jengo la makazi ya watumishi wa afya aliiomba Serikali isaidie kuboresha barabara zinazotumiwa na wakazi wa eneo hilo ili kuondoa changamoto ya usafiri kwa wagonjwa wanaokuja kuhudumiwa. Kampuni ya Pan African Energy Ltd kwa mwaka 2015 inatarajia kutumia takribani shilingi bilioni 550 kwa ajili ya kusaidia maendeleo na misaada ya huduma za kijamii katika maeneo ambayo wanaendesha shughuli zao.
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy nchini Tanzania, Patrick Rutabanzibwa akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi(hawapo pichani) kwa kuamua kutoa misaada mabalimbali katika jamii hususani mradi huu wa nyumba za Wauguzi zilizojengwa na nguvu ya wananchi pamoja na msaana mkubwa wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy katika maendeleo ya jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega akiishukuru Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy kwa kuamua kuleta misaada kwa jamii ambayo ni ya msingi hasa Hospitali pamoja na jengo la Wauguzi lililokabidhiwa katika kijiji cha Nangurukuru wilaya Kilwa
Mbunge wa Kilwa Kusini, Suleman Ally Bungara 'Bwege' (CUF) akisistiza jambo kwa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy baada ya kuona mchango wao katika jamii
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilwa Mzee Ally Mtopa akizungumza jambo
Baadhi ya Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy wakifuatilia jambo wakati wa kukabidhi jengo la Wauguzi
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy nchini Tanzania, Patrick Rutabanzibwa (wa tatu kutoka kulia) akimkabidhi funguo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega hii ni kuonesha ishara ya kukabidhiwa kwa jengo hilo la wauguzi
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Abdallah Ulega akipata maelezo baada ya kukabidhiwa nyumba ya Wauguzi iliyojengwa na Kampuni ya uchimbaji wa Gesi ya Pan African Energy nchini Tanzania
Kikundi chanyimbo za asili kikitoa burudani
Wakazi wa kijiji cha Nangurukuru nao hawakuwa nyuma wakati wa kukabidhiwa jengo la wauguzi
Watoto nao hawakuwa nyuma
Waandishi wa habari wakiwa kazini
No comments:
Post a Comment