Mgeni
rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Taifa la Sweden, Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula
akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi wa
Sweden hapa nchini. Mhe. Lennarth Hjelmaker (hayupo pichani).
Balozi
wa Sweden hapa nchini, Mhe.Balozi Lennarth Hjelmaker akifungua hafla
hiyo iliyofanyika usiku wa tarehe 09/06/2015 katika Makazi ya Balozi
huyo Masaki Jijini Dar es Salaam.
Balozi Lennarth akimkaribisha Balozi Mulamula katika hafla hiyo.
Balozi
wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Filberto Cerian Sebregondi
akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata
Mulamula huku Afisa wa Wizara hiyo Bi.Asha Mkuja (kushoto mwenye
kilemba).
Mkuu
wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchiniambaye pia ni Balozi wa
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini Mhe.Balozi Juma Halifan
Mpango akisalimiana na Balozi Liberata Mulamula.
Baadhi
ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Balozi Mulamula
(hayupo pichani)Afisa wa wizara ya Mambo ya Nje Bi.Asha Hemela
akifuatilia hotuba ya mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu Mulamula akiendelea na hotuba yake,kushoto ni Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe.Lennarth
Balozi Lennarth na
Katibu Mkuu Balozi Mulamula pamoja na wageni waalikwa wakinyanyua glasi
kutakiana kheri katika ushirikiano wa nchi hizi mbili.
Balozi
wa Sweden Mhe.Lennarth akicheza kwa furaha pamoja na wafanyakazi wa
Ubalozi huo hapa nchini kama ishara ya kufurahia maadhimisho ya siku ya
Taifa lao la Sweden sherehe zilizofanyika katika makazi ya balozi huyo
Masaki Jijini Dar es Salaam.
Kikundi
cha watoto wa Maafisa wa Ubalozi wa Sweden hapa nchini walioshiriki
hafla hiyo kwa wakiimba kwa ufasaha nyimbo za Mataifa ya Sweden na
Tanzania.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Liberata Mulamula akizungumza na Waandishi wa abari katika hafla
hiyo.Picha na Reuben Mchome.
No comments:
Post a Comment