Elimu Zetu : TANAPA Wakabidhi Jengo la Bweni la Wasichana wa Sekondari ya KISHUMUNDU ,Moshi Kilimanjaro - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 5 June 2015

Elimu Zetu : TANAPA Wakabidhi Jengo la Bweni la Wasichana wa Sekondari ya KISHUMUNDU ,Moshi Kilimanjaro




Mkuu wa mkoawa Kilimanjaro Leonidas Gama akisalimiana na baadhi ya wananchi wakati alipowasili katika shule ya sekondari Kishumundu kwa ajili ya hafla fupi ya makabidhiano jengo la Bweni la wasichana lilojengwa kwa ufadhili wa Hifadhi za Taifa Tanzania ,(TANAPA).
Viongozi mbalimbali walioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Kishumundu wakiimba wimbo wa Tanzania wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo la Bweni la wasichana lilojengwa kwa ufadhili wa Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA.
Baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia makabidhiano hayo.


Wafadhili wa shule ya sekondari Kishumundu iliyopo wilaya ya Moshi wakisalimia mara baada ya kutambulishwa katika hafla hiyo.


Mhifadhi mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Erastus Rufunguro akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Bweni la wasichana ambalo ujenzi wake umefadhiliwa na TANAPA.
Meneja Ujirani Mwema wa Hifadhi za Taifa Tanzania,TANAPA,Ahmed Mbugi akisalimia katika hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Hifadhi za Taifa,TANAPA,Ibrahimu Musa akizungumza kuhusu sera ya ujirani mwema ambayo imekuwa ikifanywa na TANAPA katika kusaidia jamii kwa nyanja mbalimbali zikiwemo za Elimu,Afya ,Miundombinu n.k
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Kishumundu wakitoa burudani ya nyimbo mbele ya wageni waliofika shuleni hapo kwa ajili ya makabidhiano ya jengo la Bweni la Wasichana lililojengwa ufadhili wa TANAPA.


Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa jengo la Bweni la wasichana katika shule ya sekondari Kishumundu,ujenzi uliofadhiliwa na Hifadhi za Taifa,Tanzania ,TANAPA.


Bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Kishumundu lilojengwa naTANAPA.


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizindua rasmi Bweni la wasichana katika shue ya sekondari Kishumundu.
RC,Gama akikata utepe kufungua jengo la Bwenila wasichana katia shule ya sekondari Kishumundu wilayani Moshi.
Sehemu ya ndani ya Bweni la wasichana katika shule ya sekondari Kishumundu,Jengo lililojengwa kwa ufadhili wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Na Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment