Benki
ya NMB imeidhinisha shilingi Bilioni 52 kama gawio kwa wanahisa wake
ikiwa ni sehemu ya faida iliyopatikana kwa mwaka 2014.Gawio hilo ni sawa
na Shilingi 104 kwa kila hisa moja na ikiwa ni ongezeko la asilimia 16
kutoka gawio la mwaka jana.
Gawio
hilo ni kutokana na faida ya shilingi Bilioni 156 baada ya kodi
iliyopatikana kwa mwaka 2014. Faida hiyo na gawio lililoidhinishwa ni
Faraja kwa wanahisa wanaojivunia benki bora yenya matawi mengi kuliko
benki yoyote Tanzania ikiwa na matawi zaidi ya matawi 163 na ATM zaidi
ya 550 huku huduma zake zikiwa zimeenea kila wilaya hapa nchini.
Gawio
hilo liliidhinishwa na bodi ya wakurugenzi na kupitishwa na wanahisa
katika mkutano mkuu wa Mwaka wa wanahisa uliofanyika siku ya jumamosi
jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas akiwasilisha mafanikio ya Benki
ya NMB pamoja na Faida iliyoipata kwa mwaka 2014 katika mkutano mkuu wa
Mwaka wa wana hisa wa benki ya NMB iliyofanyika jana jijini Dar es
Salaam. Katika Mkutano huo, bodi ya wakurugenzi ya NMB ilipitisha gawio
la Shilingi Bilioni 52 ikiwa ni gawio la shilingi 104 kwa kila hisa
likiwa ni ongezeko la asilimia 16 kutoka gawio la mwaka 2013.
Mkurugenzi
Mkuu wa NMB – Ineke Bussemaker akijibu hoja mbalimbali za wanahisa
pamoja na kujitambulisha kwa wanahisa kama mkurugenzi mkuu mpya wa benki
ya NMB katika mkutano mkuu wa wanahisa uliofanyika jumamosi jijini Dar
es Salaam. Katika Mkutano huo, bodi ya wakurugenzi ya NMB ilipitisha
gawio la Shilingi Bilioni 52 ikiwa ni gawio la shilingi 104 kwa kila
hisa na likiwa ni ongezeko la asilimia 16 kutoka gawio la mwaka 2013.
Maafisa Wakuuu kutoka vitengo mbalimbali vya NMB wakifuatilia mkutano wa wanahisa.
Mameneja wa kanda wa NMB kutoka kanda mbalimbali za benki ya NMB wakifuatilia Mkutano
Mkuu wa Wanahisa wa NMB.
Mkurugenzi
mkuu wa NMB - Ineke Bussemarker akiongea na mjumbe wa bodi ya
wakurugenzi - Mike Laisser muda mchache kabla ya mkutano wa mwaka wa
wanahisa wa NMB katika ukumbi wa Mwl Nyerere International Convention
Centre.
No comments:
Post a Comment