Biashara na Maisha : Vodacom Yalipa kodi ya Shilingi Bilioni 45.4 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Tuesday, 9 June 2015

Biashara na Maisha : Vodacom Yalipa kodi ya Shilingi Bilioni 45.4


Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza(kulia) akifanyiwa mahojiano na Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha ITV, IssaKwissa Mwaifuge baada ya kuongea na waandishi wa habari kuhusiana na mwelekeo na malengo ya kampuni ambapo alitoa takwimu za malipo ya kodi serikalini 2014/2015 ambapo alibainisha kuwa Kodi ya malipo iliyolpwa ni kiasi cha shilingi bilioni 46.4 na kukusanya kodi ya mapato, kwa niaba ya serikali kodi ya ongezeko la thamani (VAT) zaidi ya shilingi bilioni 108.6 na Kodi ya zuio inayofikia kiasi cha shilingi bilioni 81.5. kwa mwaka wa fedha uliomalizika mwezi Machi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi hao kuhusiana na mwelekeo wa kampuni ambapo pia alitoa takwimu za malipo ya kodi serikalini 2014/2015,Vodacom imelipa kodi ya mapato inayofikia shilingi bilioni 46.4 na kukusanya kodi ya mapato, kwa niaba ya serikali kodi ya ongezeko la thamani (VAT) zaidi ya shilingi bilioni 108.6 na Kodi ya zuio inayofikia kiasi cha shilingi bilioni 81.5. kwa mwaka wa fedha uliomalizika mwezi Machi.
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali Nchini wakimfatilia kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza(hayupo pichani)wakati wa mkutano na vyombo vya habari kuhusiana na mwelekeo wa kampuni ambapo pia alitoa takwimu za malipo ya kodi serikalini 2014/2015,Vodacom imelipa kodi ya mapato inayofikia shilingi bilioni 46.4 na kukusanya kodi ya mapato, kwa niaba ya serikali kodi ya ongezeko la thamani (VAT) zaidi ya shilingi bilioni 108.6 na Kodi ya zuio inayofikia kiasi cha shilingi bilioni 81.5. kwa mwaka wa fedha uliomalizika mwezi Machi.
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imelipa kodi serikalini kiasi cha shilingi bilioni 46.4 kwa mwaka wa fedha wa 2014/15 ambao ulimalizika mwezi Machi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza amesema jijini Dar es Salaam leo kuwa  mbali na kodi ya mapato,Vodacom imekusanya kwa niaba ya serikali kodi ya ongezeko la thamani (VAT)   zaidi ya shilingi  bilioni 108.6 na Kodi ya zuio inayofikia kiasi cha shilingi bilioni 81.5.
Kiasi cha kodi ya mapato iliyolipwa kwa mwaka wa fedha wa 2014/2014 ni zaidi ya shilingi bilioni 47.1 ambazo ililipa katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 na kutangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kama kampuni ya pili kwa kulipa kodi nchini na ikiwa ni kampuni ya kwanza kchania maato ya serikali katika sekta ya mawasiliano.Makampuni yaliyotangazwa kuwa ni vinara wa kulipa kodi na kukusanya kodi za serikali nchini mwaka jana ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Vodacom Tanzania na kampuni ya Sigara Tanzania .
Meza ambaye alikuwa anato taarifa ya utendaji na mwelekeo wa kampuni kwa mwaka 2014/2015 alisema “Vodacom bado imeendeleza dhamira yake ya kuendeleza sekta ya mawasiliano nchini na mpaka sasa tumewekeza kiasi cha shilingi 1.8 trilioni na katika pindi cha mwaka huu tumelenga kuwekeza zaidi shilingi bilioni 200 kwa aili ya kubresha mtandao wetu na kuboresha zaidi bidhaa na huduma zetu tunazotoa”alisema.
Aliongeza kuwa mtandao wa  Vodacom umewafikia  asilimia 99 ya watanzania kupitia minara yake 3300 iliyopo sehemu mbalimbali nchini inayowawezesha wananchi kunufaika na huduma kutoka mtandao huu bora nchini.
Meza alisema pia kuwa kampuni inajivunia huduma yake ya M-Pesa ambayo imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya kifedha nchini “Huduma hii inatumiwa na zaidi ya watanzania katika  kutuma ,kupokea fedha na kufanya mihamala ya malipo mbalimbali  na inazidi kuwarahishia maisha katika shughuli zao za ujenzi wa Taifa”alisema Meza na kuongeza kuwa M-Pesa ina mawakala zaidi ya 85,000 na imeunganshwa na mabenki 26 nchini na taasisi zaidi ya 500 zimeunganishwa na huduma hii katika  kufanya malipo na kukusanya fedha.
Katika kukuza teknolojia nchini Meza alisema Vodacom inaendelea kubuni huduma za kuwarahisishia maisha na kupata taarifa,maarifa na burudani mbalimali kupitia  mtandao wa internet.
Ili kukamilisha malengo na mikakati ya kuboresha sekta ya mawasiliano nchini kwa mwaka 2015 ameitaka serikali kutoongeza kodi kwenye sekta ya mawasiliano katika bajeti yake ya mwaka huu.Watanzania kwa sasa wanalipa asilimia 33 (kodi ya zuio na ongezeko la thamani kwa muda wa maongezi ambacho ni kiwango kikubwa katika ukanda huu wa Afrika. “Kupata mawasiliano ni moja ya haki ya msingi hivyo kuna umuhimu yanapatikana kwa kila mmoja kwa gharama nafuu”.Alisema

No comments:

Post a Comment