Na Ferdinand Shayo wa Blogu ya Wazalendo 25 Blog ,Arusha.
Wafugaji wa Vijiji vya Enduimet
na Tinga tinga vilivyopo wilaya ya
Longido mkoani Arusha wametakiwa kufuga kisasa ili waweze kuvuna mazao bora ya
maziwa na nyama ambayo watayauza na kukuza uchumi wao badala ya kujivunia
kuwa na mifugo mingi ambayo haina tija kiuchumi.
Akizungumza na Wafugaji wao kutoka
vyama vya ushirika vya Wafugaji vya Leo Pastoralist Cooperation pamoja na Tinga
Tinga pastoralist cooperation ,Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la
uhifadhi wa Mazingira na viumbe hai la African Wild life Foundation (AWF)
upande wa Hifadhi ya milima Kilimanjaro ,Noah Sitati amesema kuwa licha ya kupata manufaa ya kiuchumi wanayoyapata
wafugaji hao pia wanapaswa kuwasomesha watoto wao ili kuchochea maendeleo kwa
jamii ya Wafugaji.
Sitati amesema kuwa wako kwenye mpango
wa kuwasaidia wafugaji hao kupata madume ya kisasa yatakayowawezesha kupata
mbegu bora za ng`ombe wa maziwa na nyama hivyo kukuza uchumi wao.
“Ufugaji wa kisasa unaleta manufaa
makubwa hata ukiwa na mifugo michache ambayo utaitunza vizuri tofauti na kuwa
na idadi kubwa ya mifugo ambayo hawasaidii kuinuka kiuchumi” Alisema Sitati
Kwa upande wao Wafugaji kutoka vyama
hivyo vinavyofadhiliwa na AWF wameeleza kuwa vyama hivyo Hamisi Hassani
na Isack Ole Ndereko wamesema kuwa vyama hivyo vya usharika vinawasaidia
kuwa na sauti moja na kupiga hatua kiuchumi kupitia misaada ya kitaalamu pamoja
na fedha ambazo wanaziweka akiba na kukopeshana ili kukuza uchumi wa wafugaji.
Afisa Programu wa Shirika
la kimataifa la uhifadhi wa maliasili International Union for Consevation
of nature (IUCN) lenye makao yake nchini Kenya,Akshay
Vishwanath amesema kuwa umoja wa wafugaji utawasaidia kukuza
shughuli zao na ustawi katika kujiletea maendeleo .
Licha ya Tanzania kuwa moja kati ya
nchi zinazoongoza kwa kuwa na idadi ya mifugo bado sekta ya ufugaji nchini
haijachangia kukua kwa uchumi kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na wingi wa
mifugo,changamoto ambayo ikitatuliwa huenda sekta ya ufugaji ikakuza uchumi na
kuondoa umasikini
No comments:
Post a Comment