Kulia
ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance
Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji
wa mradi huo kwa wanahabari.Msemaji
wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa
Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public
Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani.Kulia
ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance
Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji
wa mradi huo kwa wanahabari.Baadhi ya washiriki wa semina ya Wizara ya Fedha kwa wanahabari juu ya utekelezaji wa mradi wa PFMRP.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali
Na Joachim Mushi, Dar
PROGRAMU ya
Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management
Reform Progamme – PFMRP) imetaja changamoto zinazoukabili mradi huo
licha ya mafadikio mengi iliyoyapata wakati mradi huo ukiingia awamu ya
nne ya utekelezaji wake. Mratibu wa Mradi huo ametaja changamoto hizo
leo mjini Kibaha alipokuwa akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari
pamoja na waendeshaji wa mitandao ya jamii ikiwa ni hatua ya
kushirikisha vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa mradi huo.
Mratibu
huyo alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ugumu wa kuunganisha
mifumo mbalimbali ya kifedha inayotumika serikali ili mifumo hiyo iweze
kuongea kwa pamoja, ugumu wa kujenga uwezo katika maeneo ya kitaalamu
kama E-procurement na ICTs, Uhaba wa ferdha za ndani katika kutekeleza
program na changamoto nyingine katika utekelezaji mradi.
Alisema
mradi huo unaofadhiliwa kwa pamoja na washirika wa maendeleo pamoja na
Serikali ya Tanzania tayari umeingia awamu ya nne ambapo lengo kuu la
awamu hii ni kudumisha nidhamu katika usimamizi wa Fedha za Umma na
kutoa huduma bora kwa umma ili kuleta maendeleo endelevu.
Aidha
alisema licha ya changamoto zilizopo katika utekelezaji mradi huo yapo
mafanikio hasa katika awamu ya nne ambayo ni pamoja na programu
kufanikiwa kuunganisha mfumo wa usimamizi wa fedha nchi nzima katika
serikali kuu na serikali za mitaa, kufanikiwa kufanya utafiti wa namna
Halmshauri za Wilaya/Miji inavyoweza kuongeza mapato na kufanyika kwa
zoezi la PEFA mwaka 2013 na hivyo kuibua mapungufu yaliyopo katika
usimamizi wa fedha za umma.
Mradi
pia umefanikiwa kuimarisha ushirikishaji wa utayarishaji wa bajeti
kuanzia ngazi za chini, kutumika kwa mfumo wa SBAS ambao unatoa fursa ya
kuingiza mahitaji ya Mpango wa miaka mitano na kugawa rasilimali na pia
kuchapishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa bajeti, ukaguzi mbalimbali
hivyo kuongeza kiwango cha uwazi.
Mengine
ni pamoja na kutungwa kwa sheria mpya ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya 2011
badala ya sheria iliyokuwepo Na. 21 ya 2004. Sheria hii pamoja na mambo
mengine imeiweka PPRA kutoshughulikia masuala ya michakato ya ununuzi,
na kubaki na shughuli yake kuu ya kutoa miongozo ya ununuzi wa umma.
Vile vile sheria imeongeza kiwango cha uwazi zaidi katika michakato ya
ununuzi wa umma.
"...Kujenga
uwezo wa watumishi katika kufanya kazi zao zinazohusiana na usimamizi
wa fedha za umma. Kwa mfano mafunzo kadhaa yalitolewa kwa wahasibu,
wakaguzi, wachumi; maafisa wa ununuzi...kwa lengo la kuongeza ufanisi
katika kulitumikia taifa. Kuandaa na kutoa taarifa za kifedha chini ya
mfumo wa IFMS ili kufikia vigezo vya kimataifa (IPSAS), Kuwekwa kwa
mfumo wa kusimamia mali za serikali (Asset tracking software) katiak
ofisi zote za kurugenzi ya Usimamizi wa Mali za Serikali." Alisema
Mratibu huyo.
Mafanikio
mengine ni kuongezeka kwa uwezo wa NAOT hata kufikia kiwango cha hatua
ya 3 ya AFROSAE, uhuishwaji wa mifumo ya fedha kama EPICOR ili iweze
kufanya kazi kwa ufanisi zaidi (k.m. mfumo wa EPICOR toleo la 7.3.5
ulibadilishwa na kuingizwa toleo la 9.05 wenye modules nyingi zaidi
kuliko ule wa mwanzo, Kufanyika kwa zoezi la uhamishaji wa fedha kwenda
serikali za mitaa na kuweka Mpango Kazi ili kuboresha uhamishaji wa
fedha toka serikali kuu kwenda kwenye LGAs.
Mratibu
alibainisha kwa sasa Ofisi ndogo za hazina zote nchini zimewekewa mfumo
wa IFMS, na hivyo kuongeza ufanisi, Uandaaji na utoaji wa taarifa ya
fedha za serikali kwa kutumia mfumo wa IFMS na kwa kufuata mifumo ya
kimataifa ya International Public Sector Accounting Standards Cash Basis
(IPSAS). Mradi wa PFMRP ulianzishwa mwishoni mwa miaka ya 1990, ukiwa
na lengo la kuimarisha usimamizi, kuongeza uwazi na uwajibikaji na
kujenga nidhamu ya fedha za umma katika serikali na taasisi zake, huku
ikitekelezwa sambamba na programu nyingine za kitaifa katika sekta ya
umma.
No comments:
Post a Comment