Na Dotto Mwaibale
WAPENZI
wa soka nchini sasa watafaidi kwa kutazama michuano ya kombe la dunia
chini ya miaka 20 mwaka 2015 moja wa moja kwenye luninga zao kupitia
ving’amuzi vya StarTimes pekee.
Michuano
hiyo ambayo itaanza kutimua vumbi tarehe 30 mwezi Mei na
kumalizika tarehe 20 mwezi Juni mwaka huu moja kwa moja kutoka
nchini New Zealand ambapo timu 24 za vijana kutoka mataifa mbalimbali
duniani yatachuana kuwania ubingwa.
Akizungumza
baada ya kupata haki miliki kutoka kwa FIFA za kutangaza michuano hiyo
maarufu duniani ambayo hubeba mastaa wa baadae kwa timu zao za taifa,
Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa
wanafuraha kubwa kuonyesha michuano hiyo kwani soka ni mchezo unaopendwa
zaidi duniani.
“Tunayofuraha
kubwa kuwatangazia wateja wetu kuwa tumepata haki miliki kutoka FIFA za
kuonyesha michuano ya kombe la dunia kwa vijana wa umri chini ya miaka
20 mwaka 2015 itakayofanyika nchini New Zealand. Soka ni mchezo
unaopendwa zaidi nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla na
tunaamini tutawapatia wateja wetu burudani ya matangazo yenye ubora wa
hali ya juu kupitia ving’amuzi vya StarTimes.” Alisema Bi. Hanif
“Itakuwa
ni mara ya kwanza kwa nchi ya New Zealand kuwa wenyeji wa michuano hii
ambayo inalenga kuyakusanya mataifa pamoja na kukuza umoja na amani.
Wapenzi wa soka wataweza kujionea mechi 52 kutoka kwa timu 24 tofauti.
Mchezo wa kwanza utapigwa tarehe 30 Mei ambapo utamkutanisha mwenyeji
New Zealand na Ukraine, mechi itakayoonyeshwa moja kwa moja katika
chaneli ya StarTimes Sports 2 inayopatikana katika ving’amuzi vyote vya
dishi na antenna.” Aliongezea
“Ninachoweza
kusema mwaka huu kwetu StarTimes ni wa bahati kubwa sana kwani tumeweza
kufanya maboresho makubwa katika vipindi vyetu hususani vya michezo.
Mbali na michuano hii pia kuna mingine mingi inakuja kwenye king’amuzi
hiki hivyo wapendwa wateja wetu wakae mkao wa kula,” alisema Bi. Hanif
na kumalizia, “Hivyo nawaomba wateja wetu walipie na wale wasiojiunga
wafanye hivyo sasa ili wasipitwe na uhondo huu.”
Katika
michuano hiyo bara la Afrika linawakilishwa na timu za vijana wa chini
ya miaka ishirini kutoka nchi za Senegali, Mali, Ghana na Nigeria. Huku
barani ulaya ni Ureno, Ujerumani, Austria, Ukraine, Hungary na Serbia;
kwa bara la Amerika ni Marekani, Mexico, Honduras, Panama, Colombia,
Brazil, Ajentina na Urugwai; bara la Asia ni Qatar, Myanmar,
Uzibekistani na Korea ya Kaskazini; na pia visiwa vya Fiji na New
Zealand ambao ni wenyeji wa michuano hiyo kwa mara ya
kwanza. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com
No comments:
Post a Comment