|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa kwanza kulia) kwa pamoja na
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven (wa pili kulia), Rais wa Afrika
Kusini, Mhe Jacob Zuma (wa tatu kutoka kulia), Waziri wa Mambo ya Nje wa
Burundi, Mhe. Alain Nyamitwe (wa tatu kushoto) na Katibu Mkuu wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera (wa pili
kushoto), wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kabla ya kuanza
rasmi kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki kujadili hali ya siasa na usalama nchini Burundi. Mkutano huo
ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2015. |
|
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Liberata Mulamula (wa pili kutoka kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo na Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje (kulia) nao wakiimba wimbo wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki. |
|
Dkt.
Richard Sezibera akisoma maazimio yaliyofikiwa mara baada ya Mkutano wa
Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumalizika. |
|
Kundi
la Watu Maalum la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofuatilia hali ya
siasa na usalama nchini Burundi chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Mstaafu
wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba wakifuatilia mkutano wa Wakuu wa
Nchi wa EAC. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini. |
Juu na Chini ni Wajumbe mbalimbali wakifuatilia mkutano wa wakuu wa nchi wa EAC
|
Balozi
wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Mhe. Radhia Msuya (katikati) akiwa
pamoja na Mkurugenzi Msaidizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi,
Bibi Victoria Mwakasege nao wakifuatilia mkutano
|
Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia kwa makini mkutano |
|
|
Sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini nao wakifuatilia mkutano |
|
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene (katikati) kwa pamoja na Afisa
Habari wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu Bw. Macdonald Mwakasendile
(kushoto) wakirekodi matukio |
|
Rais
Kikwete akifuraia jambo na Rais wa Afrika Kusini Mhe. Zuma pamoja na
Rais wa Uganda Mhe. Museveni mara baada ya kumaliza mkutano. |
|
Rais
Kikwete akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa
Afrika, Bi.Nkoosazana Dlamini-Zuma kabla ya kuanza mkutano. |
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe
akiongozana na Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta tayari kwenda kuanza
mkutano wa kujadili hali ya usalama nchini Burundi . |
|
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akizungumza jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya,, Bw. Vervaeke.
....Kuwasili kwa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
|
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Mulamula akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta |
|
|
Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyetta akipita kwenye Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili nchini |
|
Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe
akimtambulisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa
Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa Rais wa Uganda mara baada ya
kumpokea Rais huyo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere. |
|
Rais Museven akipita katikati ya Gwaride la heshima. |
|
Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Balozi Radhia Msuya akisalimiana na Rais wa Afrika ya Kusini alipowasili nchini |
|
Picha ya Pamoja baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Picha na Reginald Philip |
No comments:
Post a Comment