Katibu
wa Bunge Dkt. Thomas kashililah akisisitiza jambo wakati alipokutana na
ujumbe kutoka taasisi inayojishughulisha na masuala ya kibunge ya
Parliamentarians for Global Action Ofisini kwake jijini Dar es Salaam
jana. Ujumbe huo upo kwenye ziara yao ya kikazi kutembelea kila Bunge
Duniani na kueleza malengo na mipango yao hususani kuangalia namna
wanavyoweza kushirikiana na wabunge kutatua baadhi ya masuala yahusuyo
haki za Binadamu. Kulia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge Ndg. John
Joel, na kushoto ni Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Kimataifa Ndg.
Jossey Mwakasyuka na Msaidizi wa Katibu Ndg. Emmanuel Mpanda.
Katibu
Mtendaji wa taasisi ya Parliamentarians for Global Action yenye makao
makuu yake Mjini New York Marekani Dkt. David Donat Cattin akielezea
baadhi ya shughuli za taasisi yake alipokutana na Katibu wa Bunge Dkt.
Thomas Kashililah (hayupo pichani) Ofisini kwake jana Dar es Salaam.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Kimataifa la Taasisi hiyo Duniani
Mhe. Pindi Chana.
Katibu
Mtendaji wa taasisi ya Parliamentarians for Global Action yenye makao
makuu yake Mjini New York Marekani Dkt. David Donat Cattin akielezea
baadhi ya shughuli za taasisi yake alipokutana na Katibu wa Bunge Dkt.
Thomas Kashililah (hayupo pichani) Ofisini kwake jana Dar es Salaam.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Kimataifa la Taasisi hiyo Duniani
Mhe. Pindi Chana.
Kikao kinaendelea.
Katibu
wa Bunge Dkt. Thomas kashililah akimkabidhi zawadi Katibu Mtendaji wa
taasisi ya Parliamentarians for Global Action yenye makao makuu yake
Mjini New York Chini Marekani Dkt. David Donat Cattin mara baada ya
kufanya nae mazungumzo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Dkt. Cattin
walimtebelea Katibu wa Bunge kwa lengo la kueleza malengo na mipango ya
taasisi hiyo hususani kuangalia namna wanavyoweza kushirikiana na
wabunge kutatua baadhi ya masuala yahusuyo haki za Binadamu.
Na Owen Mwandumbya
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila,
amesema kila Bunge duniani lina wajibu wa kulinda na kutetea haki za
Binadamu kupitia utekelezaji wake wa majukumu yake makuu ya Kutunga
sheria, Kuisimamia serikali na pia kupitisha bajeti inayozingatiwa
mahitaji ya wananchi.
Dkt.
Kashilila ameyasema haya jumatatu wiki hii alipokutana na ujumbe kutoka
taasisi inayojishughulisha na masuala ya kibunge ijulikanayo kama
Parliamentarians for Global Action walipomtembelea Ofisini kwake ikiwa
ni sehemu ya ziara yao ya kikazi kutembelea kila Bunge Duniani na
kueleza malengo na mipango yao hususani kuangalia namna wanavyoweza
kushirikiana na wabunge kutatua baadhi ya Mmasuala yahusuyo haki za
Binadamu.
Awali
akielezea majukumu ya taasisi yake, Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo
yenye makao makuu yake nchini Marekani Dr. David Donat Cattin alisema
taasisi yake kwa kiwango kikubwa hushirikiana na Mabunge Duniani katika
kutoa taarifa na kuwahamasisha wabunge dunia kote kutetea haki za
binadamu na utawala wa sheria, Demokrasia, usalama wa binadamu, vita
dhidi ya ubaguzi, na usawa wa kijinsia kwa kuwa maeneo haya kwa kiwango
kikubwa yameigusa karibu kila jamii duniani na hususani watu wa hali
chini sana.
Alisema
kama taasisi ya kibunge duniani, wanayo kampeni mahusisi iliyozinduliwa
mwaka 2013 ambayo kwa kiwango kikubwa imesaidia kutoa elimu na msaada
wa kiufundi kwa wabunge na kuongeza utashi wa kisiasa kuunga mkono
jitihada za kutetea na kulinda haki za Binadamu duniani kwa mujibu wa
viwango vilivyowekwa kimataifa.
Pamoja
na ziara hiyo, Katibu Mtendaji huyo pia alimweleza Kashililah jinsi
taasisi yake inavyotafakari namna ambavyo itaanzisha kampeni ya kibunge
Duniani kote kupinga sheria ya kifo katika mataifa yote inakotekelezwa
sheria hii. Alisema bado wanaangalia namna bora ambayo kwa kushirikiana
na Mabunge duniani wataweza kuhamasisha serikali zote duniani kuondoa
sheria hii kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa adhabu ya kifo sio suluhu ya
makosa ama vitendo viovu katika jamii.
Akifafanua
nafasi ya Bunge katika Jamii, Dkt. Kashililah, alimweleza Katibu
Mtendaji huyo kuwa, kila Bunge Duniani lina wajibu wa kulinda na kutetea
haki za Binadamu na katika muktadha huo taasisi yake itaungwa mkono na
kila Bunge kwa kuwa inalenga kuinua ustawi wa maisha kila Mwananchi
jambo ambalo ndio jukumu la Bunge la uwakilishi.
“Wabunge
wana wajibu mkubwa katika kuhakikisha kwamba wanatunga sheria zenye
kuwawezesha kulinda haki ya kila mtu, hasa wanaoishi katika mazingira
magumu zaidi, na katika kusimamia utekelezaji wa sheria hizo”
alisisitiza Dkt. Kashililah.
Alisema
kutokana na hili, Wabunge wanayo nafasi ya kushirikiana na taasisi hii
kikamilifu hasa katika kutoa elimu juu ya kukidhi viwango vya kimataifa
katika kutetea haki za binadamu na kulinda haki za watu wote bila kujali
kijinsia na matabaka mengine.
Mapema,
Mwenyekiti wa Baraza la Kimataifa la Taasisi hiyo ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Pindi Chana
alimwelezea katibu wa Bunge jinsi taasisi hiyo ilivyoweza kusaidia
kupambana na baadhi ya sheria kandamizi katika nchi mbalimbali za Afrika
na hata Amerika ya kusini kwa lengo kuinua usawa wa kijinisa na
uwakilishi wa wanawake katika ngazi za maamuzi.
No comments:
Post a Comment