Baadhi
ya wahudhuriaji wa kongamano la kuadhimisha Miaka mitano ya mradi wa
Ujasiriamali uliokuwa unaendeshwa na Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO).
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Philippe Poinsot akizungumza wakati wa kongamano
Mshauri Mkuu wa Ufundi wa Mradi, Bwana Jealous Chirove, akielezea mafanikio ya mradi
Naibu
waziri wa kazi na ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga akimkabidhi cheti
cha kutambua mchango wa serikali ya Zanzibar katika mradi wa
ujasiriamali, ndugu Ameir Ali Ameir, ambaye ndiye Mkurugenzi wa Ajira
kutoka Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma, Zanzibar.
Mkurugenzi
wa Ajira kutoka Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma, Zanzibar.ndugu
Ameir Ali Ameir akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mkuu wa ILO Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda Bwana Alexio Musindo akizungumza na waandishi wa habari.
Naibu waziri wa kazi na ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga akizungumza na waandishi wa habari.
ILO Tanzania yaadhimisha miaka 5 ya kuwawezesha vijana Tanzania kupitia ujasiriamali. Shirika
la Kazi la Kimataifa (ILO) leo limeadhimisha miaka 5 toka kuanzishwa
kwa mfuko wa ujasiriamali wa vijana (YEF) kwa kuandaa kongamano katika
ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere.
Mfuko
wa Ujasiriamali kwa vijana ulizinduliwa mwaka 2010 ukilenga katika
kutengeneza ajira kwa vijana kwa kupitia ukuzaji wa sekta binafsi pamoja
na kuongeza ushindani kwenye uchumi wa Afrika.
Mradi
ulijikita katika kuwatengenezea vijana ajira nzuri, kukuza ujasiriamali
na kuwatengenezea fursa vijana wa kiafrika kupitia elimu, kuwaongezea
ujuzi na uwezeshaji wa mtaji. Kwa
kupitia mradi huu wa Kuwezesha Ujasiriamali, Mfuko wa Ujasiriamali kwa
vijana ulilenga kutengeneza maelfu ya ajira kwa vijana katika nchi za
Kenya, Tanzania na Uganda.
Msingi
mkuu wa mradi ulikuwa kukuza utamaduni wa ujasiriamali miongoni mwa
vijana, kuingiza elimu ya ujasiriamali katika mitaala, kuongeza uwingi
wa mambo yanayowezekana katika ajira kwa vijana, kuwezesha taasisi za
vijana kutekeleza mawazo mazuri ya ujasiriamali na kuwezesha upatikanaji
wa mitaji kwa vijana walio nje ya shule.
Toka
mradi umeanzishwa, umewezesha zaidi ya vijana 30,000 ambao ni
wajasiamarali wapya na waliopo kupitia utoaji wa elimu ya biashara,
kusaidia uanzishwaji wa biashara zaidi ya 17,000 pamoja na utengenezaji
wa zaidi ya ajira 40,000 kwa vijana, ambayo vyote kwa pamoja vimevuka
malengo ya mradi yaliyoaninishwa mwanzo.
Pamoja na hayo, mradi pia umewezesha:
· Zaidi ya biashara 16,000 zimeanzishwa ikiwa ni matokeo ya elimu ya biashara
· Zaidi ya kazi 30,000 zimetengenezwa
· Zaidi ya vijana1,000,000 wamefikiwa kupitia vyombo vya habari (radio, magazeti) na majukwaa mengineyo.
· Zaidi ya wajasiariamali 30 wa mfano wametangazwa
· Zaidi ya wanafunzi 50,000 wamepata elimu ya ujasiriamali
· Zaidi ya walimu 340 wa shule za msingi, sekondari pamoja na vyuo wameendelezwa
· Jumla ya tathmini 6 zimefanyika pamoja makongamano 3 ya kisera
· Miradi 33 imefanyika na taasisi za vijana
· Zaidi ya vijana 30,000 wamepata elimu ya biashara
Akizungumza
wakati wa kongamano, Mshauri Mkuu wa Ufundi wa Mradi, Bwana Jealous
Chirove alisema tathmini yao kwenye mradi imeonyesha kuwa zaidi ya
asilimia 50% ya vijana waliopata elimu ya biashara wameweza kuanzisha
biashara ndani ya miezi 12 huku wastani kila biashara ikitengeneza ajira
mbili.
‘Mradi
umepata mafanikio makubwa kwani kwa Tanzania pekee zaidi ya biashara
10,000 zimetengenezwa ambazo zimepelekea zaidi ya nafasi za ajira 20,000
ambazo kwa hakika ni mchango mkubwa katika kupambana na tatizo la ajira
hapa nchini’ alisema Chirove.
Mafanikio
mengine ya mradi ni uanzishwaji wa mradi wa Kazi Nje Nje ambao
unawatumia wahitimu kutoka vyuoni kuwafikia vijana walio mtaani na
ujumbe kuhusu ujasiriamali pamoja na uanzishwaji wa mashindano ya
kuandika mradi wa biashara uliowafikia moja kwa moja zaidi ya vijana
70,000.
Mgeni
rasmi wa Kongamano hili ambalo limehudhuriwa na wadau mbalimbali ni
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga amepongeza
mchango wa ILO na Mfuko wa Ujasiriamali kwa mradi wao huu.
‘Tatizo
la ajira kwa vijana bado ni changamoto kubwa kwa nchi zinazoendelea na
bara zima la Afrika kiujumla hasa kutokana na ongezeko kubwa la wahitimu
kutoka katika vyuo mbaliumbali hapa nchini, hivyo tunaishukuru ILO na
serikali ya Denmark kwa juhudi zao za kuisaidia serikali kumaliza tatizo
hili’ alisema Mheshimiwa Mahanga.
No comments:
Post a Comment