Matukio : Dk. Gharib Bilal Afungua Mkutano wa Tano wa Jumuiya ya Madola na Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa Barani Afrika, Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 26 May 2015

Matukio : Dk. Gharib Bilal Afungua Mkutano wa Tano wa Jumuiya ya Madola na Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa Barani Afrika, Jijini Dar


Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia, kufungua rasmi mkutano wa tano wa Jumuiya ya Madola na Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa Barani Afrika, uliofanyika kwenye Hoteli ya Bahari Beach, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akifurahia jambo na baadhi ya Viongozi wakati wa ufunguzi wa mkutano huo,uliofanyika kwenye Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo baada ya kufungua rasmi kwenye Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa tano wa Jumuiya ya Madola na Wakuu wa Taasisi za Kupambana na Rushwa Barani Afrika, uliofanyika Hoteli ya Bahari Beach, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment