Mradi wa Kilimo cha Tangawizi wa kikundi cha ujasiriamlai chaushindi
kilichopo katika kijiji cha Mkongotema kata ya Mkongotema tarafa ya Madaba Halmashauri ya Songea.
Na Benjamin Sawe.
Katika
ulimwengu wa sasa wenye changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira na
ushindani wa kila namna ujasiriamali unabaki kuwa dhana pekee inayoweza
kuwakomboa vijana kiuchumi na kuwawezesha kutimiza malengo na ndoto
walizonazo.
Kutokana
na kukithiri kwa idadi kubwa ya vijana wanaohitimu katika ngazi mbali
mbali za elimu hasa elimu ya msingi,sekondari na Chuo ile hali hawana
ajira na kuishia kukaa mitaani kutokana na elimu waliyoipata iliwaandaa
kuajiriwa maofisini na sio kujiajiri,ni ukweli usiopingika kwamba elimu
ya ujasiriamali inahitajika kwa kiasi kikubwa ili kuleta ukombozi wa
kweli wa kiuchumi.
Mafanikio
ni shilingi yenye pande mbili kuajiriwa na kujiajiri ,vijana wasifikiri
kuwa kuajiriwa ndio njia pekee ya kufanikiwa pia wajue kuwa kuna
mafanikio ya kiuchumi nje ya ajira na haya ni kwa wale walioamua
kujiajiri kwa kuanzisha miradi mbali mbali ama biashara na huo ndio
ujasiriamali wenyewe.
Vijana
wengi wamekuwa wakihuzunika, kunung’unika na kulalamika kana kwamba
waliambiwa maisha ni rahisi. Wakati unapoukubali ukweli ya kuwa maisha
ni magumu, ndiyo wakati ambao maisha hayawi magumu tena! Ndiyo! Kwa
sababu ukijua maisha ni magumu lazima utaishi kwa nidhamu kubwa, na
nidhamu ndiyo msingi namba moja wa kutatua matatizo yote katika maisha.
Ukiona
unalalamika kuwa maisha ni magumu, rejea katika fikra zako, huenda bado
hakujafanyika mapinduzi! Ukiona unaukubali ukweli kuwa maisha ni magumu
na wakati huo huo huna nidhamu, ama una nidhamu chache, basi ujue kuwa
hujaukubali ukweli wote kuwa maisha ni magumu!
Ujasiriamali
kwa ujumla ni dhana ambayo ili kukubalika kikamilifu, kunahitajika
mapinduzi makubwa ya fikra kwa vijana kuliko elimu ya kawaida. Fikra za
kuwatazama wajasiriamali waliofanikiwa na kutoa visingizio kuhusu
mafanikio yao, ni fikra zenye matege na ukilemaa na hizo kamwe haziwezi
kutufanya tukafanikisha kujikwamua kiuchumi.
Kutokana
na hali hii, utagundua kuwa tatizo linalowakabili vijana wengi wa
Tanzania katika kujikwamua kiuchumi si mitaji wala ukosefu wa elimu,
bali ni la kifikra.
Ili
kijana aweze kufanikiwa kubuni na kuanzisha mradi, anatakiwa aamini kuwa
kujiajiri kuna tija kubwa sawa na kuajiriwa. Kwa sababu ni mara chache
mtu anaweza kuwa tajiri kwa kutegemea mshahara wake pekee!
Ni
vema vijana wote wafahamu kuwa “fedha ni mawazo.” Kama fedha ni mawazo
basi kujikwamua kiuchumi ni mawazo pia. Kama ni suala la kuwaza, kwa
nini asiye na elimu asiwaze? Kama ujasiriamali unaanza na mawazo, kwa
nini wenye elimu walilie mitaji? Sikatai kuwa mitaji ni suala la msingi
katika ujasiriamali, lakini ifahamike kuwa uthubutu wa kuanza na
kujaribu wazo hata kwa sehemu ndogo ndiyo msingi wa mafanikio ya
mjasiriamali yeyote.
Nchi
ya Tanzania ina ajira na fursa nyingi za kiuchumi za kumtosha hata mtoto
atakayezaliwa kesho! Sioni sababu ya mhitimu wa darasa la saba kukosa
ajira, kwanini mhitimu wa kidato cha nne na sita wakose kitu cha kufanya
chenye kuwakwamua kiuchumi katika nchi tajiri kama Tanzania? Kwa wale
ambao ni wahitimu wa vyuo vya kati na vya elimu ya juu, sioni haja ya
kuwaandikia kwa sababu inatosha sana kwao kutengeneza ajira kwa wengine.
Tatizo
jingine linalowasibu vijana wengi wa Tanzania kiasi cha kushindwa
kupoka (seizing) fursa za kijasiriamali na fikra potofu za kutaka kuanza
na mafanikio. Kama ni kijana msomi anawaza kuanza na kampuni yenye
mtaji wa mamilioni. Yatatoka wapi mamilioni bila kuanza na kidogo? Kwa
wale ambao hawana elimu kubwa wengi wamevia kimawazo kwa kuota kuokota
fedha ama kuokota elimu!
Kama
ulikosa elimu hupaswi kulalamika wala kunung’unika kwa sababu huko ni
kupoteza muda, bado unayo nafasi kubwa ya kufanikiwa. Fikra za kupata
vya bure bila kuhangaika ndiyo zinazosababisha Watanzania wengi
kujiingiza katika michezo mingi ya bahati nasibu kwa matarajio kuwa
watatoka! Cha ajabu ni kuwa michezo hiyo, ama mingineyo inawapotezea
fedha badala ya kuwasaidia, hapa yanahitajika mapinduzi ya kifikra.
Maisha
bora na ya uhakika kwa vijana yanawezekana ikiwa kutafanyika mageuzi
makubwa katika sekta binafsi, ujasiriamali. Ili ujasiriamali ufanikiwe
na kufanywa na vijana kwa uhakika, lazima vijana wote wakubali kufanya
mapinduzi ya fikra zao za kitegemezi.
Tukisema
ujasiriamali hatumaanishi ujasiriamali wa kujikwamua wewe kijana peke
yako, bali tunagusa pia katika utanuzi wa fikra za kuanzisha kampuni,
huduma na bidhaa mbalimbali zenye ubunifu mpya kwa kuvitumia vipaji
kikamilifu.
Vijana
wengi wamekuwa wakilalamikia ugumu wa maisha na kuacha kujishughulisha
na ujasiriamali hivyo kupelekea kukabiliana na ugumu wa maisha.
Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za Sheria Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Ester Riwa akitoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wa mkoa
wa Ruvuma anasema vijana wengi nchini wamekuwa wakitaka kupatiwa pesa
bila kuzingatia mafunzo ya elimu ya ujasiriamali hivyo kupelekea upotevu
na usumbufu katika urejeshaji wa marejesho.
Anasema
baadhi ya vikundi vya vijana katika Halmashauri mbalimbali wamekuwa
wakigomea mafunzo ya ujasiriamali na kudai posho za mafunzo na kusahau
mafunzo wanayapatiwa ni muhimu kuliko hiyo poshowanayodai.
Bi
Riwa anasema Serikali haitoi posho za mafunzo ya ujasiriamali bali hutoa
elimu na baadae kutoa mikopo kwa vikundi vilivyosajiliwa kisheria.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa Mh.Norman King anasema Serikali imeamua kutoa mafunzo kwa
vikundi vya vijana ya jinsi ya kuandaa maandiko ya miradi mbalimbali,
uongozi bora na stadi za maisha ili kuwatoa katika mitazamo hasi kwenda
mitazamo chanya kwa kutumia fursa zilizopo.
Anasema
vijana wengi wanafursa mbalimbali za kujikwamua na umaskini lakini
hawatumii fursa hizo vizuri na kubakia wakikaa vijiweni bila
kujishughulisha na kazi yeyote na kuishia kuvuta madawa ya kulevya na
kuwa wezi.
Nea
Diwani wa kata ya Matimila jimbo la Peramiho Mh. Menesi Komba amesema
mafunzo ya kujengewa uwezo ni fursa kwa vijana wa Halmashauri ya Songea
kwani watakuwa wamepewa uelewa mkubwa wa jinsi ya kuendesha shughuli zao
za ujasiriamali kwa ufanisi na utaalamu
Anawaasa
vijana kutekeleza elimu ya ujasiriamalikwa vitendo kwa kuwafundisha
vijana wenzao ambao hawakupata bahati ya kuhudhuria katika mafunzo hayo
na kuachana na tabia ya kuwa wabinafsi wa kutoa elimu ya ujasiriamali
kwa vikundi vingine.
Tubadili
mitazamo ya kuwaona ni sehemu ya matatizo katika jamii bali tuwaone
kama ni sehemu ya suluhisho la matatizo yaliyopo kwenye jamii kwasababu
vijana wana nguvu,vipaji,uwezo wa ajabu,ubunifu .
Nguvu za vijana zikitumika vizuri zinaweza kufukuzisha umasikini,utegemezi na matatizo lukuki yanayoikumba jamii.
Vijana
nao wasikae nyuma katika masuala ya kifamilia ,kijamii,wawajibike
watumie nguvu walizonazo,ubunifu,uwezo,vipaji na talanta na elimu
walizonazo katika kutatua changamoto za jamii badala ya kukaa kama watu
wa pembezoni.
Ni
vyema kuhamasisha ushiriki mpana wa vijana katika masuala ya
kiuchumi,kijamii na kisiasa kwasababu vijana wakiachwa nyuma hali
itazidi kuwa mbaya kwa vizazi vijavyo.
“Nusu
ya maisha tunayoishi yanatokana na kizazi kilichopita na nusu nyingine
inatokana na kizazi kilichopo” Anaeleza Mtunzi mmoja wa kitabu.
Ina
maana kuwa vijana wanawajibika kuweka misingi bora ya kiuchumi,kimaadili
na kiuwajibika misingi ambayo itatumiwa na kizazi kijacho iwapo
hawatafanya hivyo hali itazidi kuwa mbaya .
“Unapoacha
kutimiza wajibu wako duniani,kutumia uwezo ulionao,vipaji unapokufa
unaacha nafasi wazi duniani ambayo ingepaswa uijaze kwa kuacha kitu
duniani kizazi kijacho kikija kitakuta nafasi uliyoiacha hukufanya kitu”
Anaeleza Mtunzi Mashuri wa vitabu Myles Munroe.
No comments:
Post a Comment