Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendeshwa na
kampuni ya Proin Promotion linalolenga kuinua vipaji kwa vijana ikiwa ni katika
kuwatengenezea mazingira ya ajira katika maisha yao Nchi nzima kikanda
lionekana kuwa msaada kwa vijana wengi waliokuwa wakijitokeza kushiriki
mashindano hayo katika mikoa mbalimbali tulikopita.
Shindano la ya Tanzania
Movie Talents msimu wa pili 2015 lilioanza
mwezi Aprili kikanda kwa kuanza na kanda ya ziwa mwanza, Kanda ya kaskazini
Arusha,Kanda ya kati Dodoma na kisha kanda ya nyanda za juu kusini Mbeya limekamilika
kwa siku ya jana kupatikana washindi watatu na kujinyakulia kitita cha shilingi
laki tano kila mmoja kati ya washiriki mia tatu waliojitokeza kushindana
Jana jioni Jijini Mbeya
Soko Matola Mkapa Conference Center ndipo mashindano hayo yalipofanyika na
kuhudhuliwa na vijana kutoka wiraya zote za mkoa wa Mbeya na mikoa ya jirani kama
Iringa na mikoa mingine ya jirani.
Washindi hao watatu
watakwenda kuungana na wenzao wa kutoka kanda zote nchini kwa kuingia kwenye
nyumba ya TMT wakifundishwa sanaa na waalimu mbali mbali kutoka Chuo kikuu
Mlimani,kisha kuwepo na mtoano wa kila wiki ilikubaki washiriki kumi na mwisho
kupata mmoja atakayeibuka na shilling Milioni Hamsini za kitanzani,hao kumi watakao
baki wataigiza movie ya pamoja ikiwa ni katika kuwatambulisha katika tasni ya
sanaa nchini ili iwe ajira kwako.
Baada ya kutoka Jijini Mbeya
ni Mtwara tarehe 26 na 27 mwezi huu kisha Dar es salaam 5-7 mwezi wa 6,kwa
taraifa zaidi tazama ITV na sikiliza Redio one au redio za mkoa husika kujua
taharifa zaidi za mahala na muda.
|
Meza ya kufanya usajili kabla ya kuingia ndani kuonesha kipaji chako kwa majaji wa TMT |
|
Foleni ya wasanii wa Mkoa wa mbeya waliojitokeza kuchukua form kujisajili katika Shindano hilo |
|
Foleni ya wasanii wa Mkoa wa mbeya waliojitokeza kuchukua form kujisajili katika Shindano hilo |
|
Wasanii wa Mkoa wa Mbeya walipokuwa wakipewa maelezo na kuuliza maswali kuhusu shindano la TMT |
|
Msaani
maarufu wa Bongo Movie Mboto ni mmoja wa team ya TMT katika kuwapa
maelekezo wasanii waliojitokeza kushiriki shindano hilo |
|
Mpaka Kieleweke....!!!!!! |
|
Majaji wa TMT Rich,Monalisa na Roy katika meza yao wakitazama na kujaji vipaji vya wasanii waliojitokeza katika mashindano |
|
Mboto akiwa kazini
|
Meneja
wa mradi wa TMT 2015 Saul Mpoki akizungumza na wasanii wa mkoa wa Mbeya
kuhusu makusudio ya mradi huu katika kukukuza vipaji vyao na
kuwatengenezea mwanya wa ajira.
|
Jaji Mkuu Roy akitoa maelekezo namna ya kuigiza kwa kutumia mswada (script) kuusoma na kuuelewa vizuri |
|
Washiriki wakiwa mbele ya majaji wakipewa maelekezo namna ya kuigiza kwa kutumia mswada (script) hasahasa kuusoma na kuuelewa. |
|
Washiriki wakisoma mswada (script) na kuigiza kabla ya kwenda kwa majaji kuonesha uwezo wao |
|
Washiriki wakisoma mswada (script) na kuigiza |
|
Washiriki wakisoma mswada (script) na kuigiza kabla ya kwenda kwa majaji kuonesha uwezo wao |
|
Baada ya kusoma Script wanasubiri kuingia ndani kwa majaji kuonesha ujuzi wao katika kuigiza kutumia mswada (script) |
|
foleni kuingia ndani kwa majaji kuonesha ujuzi wao katika kuigiza kutumia mswada (script) |
|
Majaji watatu wa TMT 2015 |
No comments:
Post a Comment