Mshindi
wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamisi Khalid (kushoto) mkazi wa
Mtwara akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati
wa hafla ya kukabidhiwa hundi yake na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na
Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kulia) baada ya
kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo hafla hiyo
ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es
Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Mshindi
wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamisi Khalid (kushoto) mkazi wa
Mtwara akikabidhiwa hundi yake na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na
Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia wakati wa hafla ya
kukabidhiwa hundi hiyo baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia
promosheni hiyo. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo
mlimani city jijini Dar es Salaam. Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Rosalynn
Mworia ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania (kulia) akimpongeza kwa kumpigia makofi mshindi wa kitita cha
shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa
na kampuni hiyo, Hamisi Khalid (aliyeshikilia hundi) mkazi wa Mtwara
wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi hiyo baada ya kuibuka mshindi wa
kitita hicho kupitia promosheni hiyo. Hafla hiyo ilifanyika Makao makuu
ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn
Mworia (kulia) akisoma tarakimu kwenye hundi yenye thamani ya shilingi
milioni 100/- wakati wa hafla ya kumkabidhi hundi hiyo mshindi wa kitita
cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamisi Khalid (aliyeshikilia hundi)
baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo. Hafla
hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es
Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Mshindi mwingine wa milioni 100 za Jaymillions akabidhiwa kitita chake
v Ni mjasiriamali na mkazi wa Mtwara
v Wateja watakiwa kutuma neno JAY kwenda 15544
Mshindi wa pili wa milioni 100/- katika promosheni ya JayMillions
inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hamis Khalidi (30) mkazi wa mkoani
Mtwara na mjasiriamali anayeuza vifaa vya saluni za kike leo
amekabidhiwa fedha zake katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam
ambako amefungua akaunti.
Promosheni ya JayMillions inayoendelea ikiwa inakaribia kufikia mwisho
mnamo Aprili 23, 2015 imekwishawawezesha baadhi ya wateja wa Vodacom
kuwa mamilionea kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha na
maisha kuwa murua na hadi kufikia sasa wamekwishapatikana washindi
wawili wa milioni 100/-, washindi wanne wa milioni 10/- na washindi 39
wa milioni 1/-. Maelfu ya wateja pia wamejishindia muda wa maongezi.
Washindi wa milioni 100/- ni Uwezo Madegenge kutoka wilayani Kilolo
mkoani Iringa na Hamis Khalidi ambaye amekabidhiwa kitita
alichojishindia. Washindi wa milioni 10/- ni Zuena Rajabu mkazi wa
Segerea , Hyness Petro Kanumba kutoka Rukwa, James Mangu (Mwanza), na
Deborah Stanley mkazi wa Kimara kwa Komba jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati akikabidhiwa fedha zake za Ushindi, mshindi wa
shilingi milioni 100 wa promosheni hiyo, Hamis Khalid, amewaomba
Watanzania kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Vodacom Tanzania katika
kujenga na kuimarisha maisha ya Watanzania.
"Nimefuatilia Promosheni ya Jaymillions naona inalenga kuwakomboa
kimaisha Watanzania hususani wenye kipato cha chini hasa wajasiriamali
wadogo wadogo kama vile; wamachinga, mama ntilie, na pia wastaafu ambapo
kwa kiasi kikubwa tunajua watu wa matabaka haya wanahitaji msaada ili
kujiendeleza kiuchumi. Kwa fedha ambazo baadhi ya washindi tayari
wamezipata wengi zimewasaidia kujikwamua na kujiendeleza kimaisha," alisema Khamis.
Aliongeza kuwa yeye ni mfano dhahiri wa Watanzania kuwa promosheni hii
haina ujanja bali ya kweli kwa kuwa pamoja na kuishi mkoani ameweza
kushinda na leo ameingiziwa fedha zake kwenye akaunti. "Sasa nimepata
mwanga katika maisha yangu baada ya kujishindia fedha hizi kwa sababu
sijapewa masharti wala utaratibu wowote wa matumizi ya fedha hizi,
maisha niliyokuwa nayo yalikuwa ya kuhangaika sana kutokana na kuwa na
mtaji mdogo na sasa yamewezeshwa na promosheni hii’’.Alisema.
Khalid alisema kwa fedha hizi alizojishindia anaona tayari ameanza
safari ya kuwa mfanyabiashara mkubwa mwenye mafanikio kwa kuwa
ataimarisha biashara yake na kufungua miradi mbalimbali ikiwemo kusaidia
familia yake ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha.
Aliongeza kuwa ana matarajio ya kutoa msaada katika vituo vya watoto
yatima kama njia yake ya kutoa shukrani kwa ushindi huu ambao
umebadilisha maisha yake.
Akizungumza katika hafla iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo, Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rosalynn
Mworia aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya JayMillions
ili wajishindie mamilioni ya fedha kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY
kwenda namba 15544 ili kutopoteza bahati zao za kushinda.
Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba
15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa
shilingi 300/- tu.
“Tunaendelea kuwasisitizia wateja wetu wacheki kila siku ili kujua
kama namba zao zimeshinda hasa kipindi hiki ambacho promosheni inaelekea
ukingoni. Kama Khalid asingetuma ujumbe siku ile angeendelea tu na
maisha yake kama yalivyokuwa bila kujua kama namba yake ilichaguliwa
kushinda kwa maana bado kuna mamilioni ya kushinda yanayoweza
kubadilisha maisha ya wateja wetu,” alisema Mworia.
Mbali na kumkabidhi zawadi yake nono hiyo, kampuni ya Vodacom inamsaidia
Hamis kupata mafunzo ya ujasiriamali na matumizi sahihi ya ili
kumuwezesha kufanya matumizi yenye tija.
No comments:
Post a Comment